Posted by Esta Malibiche on Oct8.2016 in NEWS
Mbunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi CCM Ridhiwani Kikwete akimkabidhi magodoro 2000 mkuu wa shule ya Sekondari Moreto Mwalimu Lyamuya
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amekabidhi Magodoro 200 katika shule ya Sekondari Moreto ikiwa ni moja ya ahadi yake aliyoitoa Oct6 2016 na leo oct8.20 ameitekleleza.
Mhe Ridhiwani Kikwete aliitoa ahadi hiyokutoknana na bweni la shule hiyo kuteketea kwa moto Oct4.2016ambapo alitembelea shule hiyo na kuahidi kutoa magodoro ili yaweze kuwasaidia wanafunzi waliopafikwa na maafa hayo
Akikabishi godoro hizo kwa mkuu wa shule hiyo Mwalimu Lyamuya,Mhe.Ridhiwani aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri mitihani yao na hatimae kufauru na kujiunga na Elimu ya juu.
Aidha aliwasihi kuepukana na vishawishi ambavyo vinaweza kuwaharibia masoma yao na hatimae kushindwa kutimiza ndoto zao za baadae.
'''''Ninawaomba mzingatie masomo,kile mnachofundishwa darasani mkifanyie kazi ili baadae muweze kuwa viongozi wazuri .Someni kwa bidii,pia akili zenu zote zielekee katika masomo ili muweze kufauru vizuri na hatimae jimbo letu liweze kuwa na wasomi wazuri na si vinginevyo ''''''alisema Ridhiwani.
0 maoni:
Chapisha Maoni