Posted by Esta Malibiche onOct9.2016 in NEWS with No Comment
|
Askofu
wa doyosisi ya Iringa Dr Mdegela kulia akimtambulisha rasmi askofu
mteule wa dayosisi hiyo mchungaji Blaston Gavile na mkewe mbele ya
waumini wa kanisa kuu leo |
ASKOFU
wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegela
amewapongeza waumini wa dayosisi hiyo kwa kumpata
askofu mpya atakayechukua nafasi yake pasipo
kuwepo kwa vurugu za aina yoyote tofauti na
maeneo mengine ambayo pindi linapotokea zoezi la
uchaguzi wa askofu huwa na vurugu kubwa .
Askofu Dr Mdegela aliyasema hayo leo katika Ibada
maalum ya kumtambulisha askofu mteule mchungaji Blaston
Gavile na msaidizi wake Himid Saga uliofanyika katika
kanisa hilo usharika wa Kanisa kuu,
alisema kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika ijumaa umemalizika kwa
amani na utulivu mwingi na kupelekea
heshima kubwa kwa dayosisi ya Iringa na Tanzania kwa ujumla .
"
Tumemaliza uchaguzi wetu kwa amani na utulivu
mwingi na hadi sasa hapa nimepokea salamu za
pongezi kutoka Dayosisi mbali mbali na hata nje ya
Tanzania wakipongeza kwa jambo hilo
kufanyika pasipo kuwepo kwa vurugu zozote ....hii ni
heshima kuwa imewekwa na yote haya yamewezekana
kutokana na kazi nzuri ya waumini kufanya maombi "
Alisema
kuwa hakuna jambo lolote alilolifanya vema
pasipo kumtanguliza roho mtakatifu hivyo
ombi lake kwa wale waliopewa kazi na Mungu ya kuongoza
dayosisi hiyo ni kuepuka kusikiliza maneno ya
watu wanayoyasema barabarani na badala yake
kumtanguliza Mungu na kusikiliza kile kinachosemwa
na viongozi wa dayosisi kwani maneno ya mitaani
ni ya hivyo hivyo.
" Mimi
yamesemwa mengi ila nawasamehe bure wale
wote waliosema ila nawaomba baadae wote wakatubu wapo
ambao walikuwa wakifanya kazi ya kunichafua katika
vyombo vya habari na mitaani kwa kusema mambo ya aibu dhidi
yangu ila kiuharisia sivyo hivyo ....kuna wengine ni
maaskofu walipata kutamka kuwa mimi natumia
vibaya fedha za chuo kikuu cha Iringa
wakati wao ni wasomi na wanajua kabisa kuwa
chuo kinakaguliwa na kuna taratibu nzuri tu
za kifedha ila kwa kuwa walikuwa wanafanya hivyo kwa
kufurahisha nafsi zao na kupotosha nasema ni
wakati wa wote kutubu na wakitubu waje kuniomba msamaha
"
Akifafanua
juu ya ajenda ya waumini wa Kanisa hilo jimbo la
Mufindi kutaka kuhama Dayosisi yao ya Kusini na
kuhamia Dayosisi ya Iringa alisema kuwa kuwa
ajenda hiyo ilizungumzwa na aliyewasilisha ajenda
kwenye mkutano mkuu huo alikuwa ni yeye mwenyewe.
" wapo
watu wanapotosha kuwa ajenda ya Mufindi kuhamia
Dayosisi ya Iringa hakuzungumzwa kwenye mkutano mkuu
nawaambia kuwa ajenda hiyo imezungumza na mimi
ndie niliyeiwasilisha usiku wa octoba 6 mbele ya
wajumbe kwa kutoa maelezo maana ajenda ya askofu
ni ajenda ya mkutano mkuu hivyo
sikuipeleka Halmashauri kuu wala kamati ya
utendaji nilitoa taarifa kwenye mkutano
huo kuwa Mufindi wameamua kuhamia Iringa
tulipowauliza kuwa wanataka dayosisi walisema hapana
wao wameamua kuhamia Dayosisi ya Iringa hivyo
niliwaambia wajumbe kuwa hamuwezi ninyi kuwaambia
wasihamie maana dayosisi ni mali ya Mungu si mali
ya mwanadamu na wakihamia kuhamia popote wao
wanaweza hivyo wajumbe wa mkutano huo walikubali kuwapokea
..... hoja ya pili wajumbe walisema kutokana na
jambo hilo kuwa bado linasumbua kanisa
waliniomba mimi Mdegela kuendelea kuliratibu jambo
hilo hadi mwisho ila kuna uzushi
umetokea kuwa katibu mkuu anasema ajenda hiyo
haikuwepo ni kweli kabisa ajenda kubwa ilikuwa ni uchaguzi mkuu
lakini ile nilisimama nikasema kama mimi kwa hiyo
mimi nawajibika kusema mbele ya wajumbe na pia
nawajibika kubaki na majibu ya ule mkutano mkuu
yanayosema maamuzi ya waumini wa Mufindi ndio
tutakaouheshimu ndio kauli ya mkutano mkuu "
Askofu
Dkt Mdegela alisema kuwa watu wanasema kuwa
msemaji wa dayosisi ya Iringa ni katibu mkuu wapo hao ni
wapotoshaji na wanapaswa kupuuzwa kwani
hadi sasa yeye Askofu ni msemaji mkuu wa
dayosisi ya Iringa hadi hapo januari mwakani siku
ambayo askofu mpya atasimikwa rasmi japo
katibu mkuu anapaswa kusema kwa ruksa
kutoka kwake hivyo anawataka waumini wa jimbo la Mafinga
kupokea majibu ya maombi yao kuwa yamepokelewa rasmi .
Alisema kuwa waumini wa Mufindi waliomba kuhamia dayosisi
ya Iringa baada ya kudai kuwa hawapendi kuendelea kubaki
dayosisi ya kusini na hivyo walikuwa njia panda kwanza
iwapo wangekataliwa Irinda walipanga kuanzisha kanisa
lao ama kuanzisha dayosisi yao lakini si kubaki dayosisi ya
Kusini .
" Mimi ni mtaalam wa Imani
hivyo niliwajibu kwa barua kuwa cha kwanza kuwapatanisha na
katibu mkuu na askofu wa dayosisi ya kusini
pia kuombana msamaha pale walipokosana ......mimi
sina chuki hata kidogo na askofu mwenzangu wa
kusini Mengele amekuwa ni rafiki yangu siku
zote walipokosana wakristo wa Mufindi na askofu wao
Mengele ni pale walipokamatwa na kuwekwa mahabusu
kijiji cha Mdandu na kunyimwa dhamana na kukosa
kushiriki mkutano mkuu ambayo ni mamlaka kuu ya dayosisi na
Halmashauri kubaki kimya juu ya suala hilo
sasa mimi nasimamia ukweli kuwa mimi kama askofu
sikutumwa kufunga watu polisi nimetumwa kuwakomboa wakristo
ndio wanaochagua viongozi na wanayohaki ya kusikilizwa
sio kufungwa gerezani sasa kama haya
yanamkwaza mwenzangu sina jinsi huu ndio
ukweli lakini tujiulize kama Yesu angewakuta pale mahabusu
mdandu angefanya nini "
0 maoni:
Chapisha Maoni