Posted by Esta Malibiche on Oct15.2016 in NEWS
Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,
Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, akiwa na
Mkuu wa wilaya ya Igunga na viongozi mbalimbali akipewa taarifa juu ya
ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na vyoo vya shule za sekondari
wilayani humo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,
Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, akipewa
maelekezo juu ya matumizi ya mfumo wa kukusanyia mapato.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,
Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, akiwa na
mbunge wa Nzega Hussein Bashe katika ukaguzi wa bweni la wasichana
wilaya ya Nzega.
………………………………………………………………………
KUTOKANA na baadhi ya wananchi
kuwafanyia vitendo vya ushirikina watumishi katika Halmashauri
mbalimbali nchini, Naibu Waziri Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na
serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ameonyeshwa kukerwa na tabia
hiyo huku vimesababisha watumishi kupata msongo wa mawazo na wengine
kuomba kuhamishwa.
Jafo alitoa kauli hiyo alipokuwa
akikagua zahanati mpya iliyopo kijiji cha Ziba ndani ya Jimbo la Manonga
wilayani Igunga mkoani Tabora na alipokuwa akizungumza na watumishi wa
wilaya hiyo.
Alimuagiza mkuu wa wilaya ya
Igunga kutenga muda yeye na kamati yake ya ulinzi na usalama
kuwafikishia ujumbe wananchi wa wilaya ya Igunga kuwakemea wenzao wenye
tabia hiyo wilayani humo ili kuacha tabia hiyo ovu.
Jafo alisisitiza kwamba tabia
hiyo imewasababishia baadhi ya watumishi walio tendewa vitendo visivyo
kupatwa na msongo wa mawazo na kuomba kuhama maeneo walio pangiwa.
Naibu Waziri alisema kwamba jamii
inapaswa kuwathamini watumishi kwani wametoka maeneo mbalimbali ya nchi
ili kuja kuwatumikia wao hivyo wanatakiwa kuwathamini na kuwaheshimu
kwa kulinda utu wao.
” Watani zangu mliopo hapa
Wasukuma na Wanyamwezi mmepata zahanati nzuri naomba muitunze. Pia
sitaki kusikia daktari au mhudumu amelala asubuhi anajikuta ng’ambo ya
barabara au katika kiwanja cha mpira,”alisema Jafo
Kadhalika, alikemea kitendo cha
sungusungu walio mchapa viboko mwalimu mkoani humo huku akiwaagiza wakuu
wa wilaya maeneo yote kupambana na tabia za udhalilishaji wanazo
fanyiwa watumishi wa umma katika jamii ili waweze kufanya kazi kwa amani
na kujiamini.
Aliwapongeza viongozi wa mkoa wa Tabora kwa umoja na ushirikiano wao katika kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni