Baada
ya kujitokeza tukio la mashabiki wa Simba kuvunja viti vya Uwanja wa
Taifa katika mchezo wa Yanga na Simba kisha Rais John Magufuli kuelezea
masikitiko yake kwa kile kilichojitokeza katika mchezo huo, klabu ya
Simba imejitokeza na kumuomba rais msamaha.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema klabu
inakubali kufanya kosa hilo na kwa pamoja kuanzia rais hadi mashabiki
wanaomba msamaha kwa Rais Magufuli na kuahidi jambo hilo halitajitokeza
tena.
“Rais
wa klabu ya Simba, kamati ya utendaji, sekretarieti, benchi la ufundi
na wachezaji, wanachama na mashabiki wa Simba wanaomba radhi kwa Rais wa
Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya
michezo, Nape Nnauye kwa kitendo kisicho cha kiungwana kilichofanywa na
mashabiki wetu katika mchezo wa Yanga,
“Tumeona
twende mbali na tumwombe radhi rais wetu, hizi ni rasirimali zetu,
zinajengwa na kodi zetu, serikali inatumia gharama za kubwa kuziendeleza
rasirimali hizi, ni upuuzi wa hali ya juu kabisa kufanyika kitendo kama
kile,” alisema Manara.
Msemaji
wa Simba Haji Manara akielezea goli la Amissi Tambwe katika mchezo wa
watani wa jadi, Simba na Yanga uliopigwa Jumamosi ya Oktoba mosi katika
dimba la Uwanja wa Taifa na kumalizika kwa kufangana goli moja kwa moja.
Aidha
Manara amesema klabu ya Simba inaamini serikali itawaruhusu tena
kuendelea kutumia uwanja wa taifa na kwa wanachama wote ambao
watabainika kufanya uharibifu ule watachukuliwa hatua za kisheria.
“Tunaamini
serikali itarudi nyuma na kuturuhusu kutumia uwanja wa taifa na katika
hili tunaahidi tukio kama lile halitajitokeza tena, na kama klabu
itabaini kuwa kuna wanachama wetu walishiriki kufanya tukio lile
watachukuliwa hatua,
“Na
tunaiomba serikali ifungue zile kamera za CCTV pale uwanjani ili tukio
kama lile likijitokeza iwe rahisi kuwabaini waharifu waliohusika, ule ni
uharifu wa makusudi, leo klabu inapata hasara, tunahangaika kufanya
vikao mara wizara mara shirikisho kwa ajili ya watu wachache,” alisema
Manara.
0 maoni:
Chapisha Maoni