Mwenyekiti wa Mkutano wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ambaye ni
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo
kwenye mkutano huo wa siku mbili unaofanyika mjini Unguja visiwani
Zanzibar.
Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC Bw. Salum Kassim Ali, akieleza
jambo kwenye mkutano huo wa siku mbili unaofanyika mjini Unguja visiwani
Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel Kawishe akifafanua jambo
kwenye Mkutano wa NEC na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
unaofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar.Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa
NEC Suleiman Balula.
Afisa Uandikishaji Msaidizi wa
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Kati Unguja, Bw. Mbaraka
Said Hassuni ambaye ni Mwanasheria akichangia jambo kwenye Mkutano kati
ya NEC na ZEC unaofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya
Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Giveness Aswile
akichangia jambo kwenye Mkutano kati ya NEC na Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC) unaofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar.
Baadhi ya Maafisa wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
wakifuatilia uwasilishaji wa masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
tume hizo kwenye mkutano unaofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar.
Baadhi ya Maafisa wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
wakifuatilia uwasilishaji wa masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
tume hizo kwenye mkutano unaofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar.
………………………………………………………………….
Hussein Makame, NEC-Zanzibar
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imekutana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ili kuimarisha uhusiano na
kubadikishana uzoefu katika kuboresha utekelezaji majukumu ya tume hizo.
Baadhi ya mambo ya ambayo tume
hizo zinashirikiana ni utekelezaji wa mkakati wa utoaji wa elimu ya
mpiga kura na marekebisho ya Sheria mbalimbali.
Mkutano huo wa siku mbili
unafanyika mjini Unguja na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka pande zote
mbili na kuongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima
Ramadhani.
Katika mkutano huo Bw. Kailima
ilieeleza jinsi NEC ilivyoshiriki katika kutoa elimu ya mpiga kura na
kuelimisha wadau wa uchaguzi na wananchi juu ya taratibu za uchaguzi na
majukumu ya Tume hiyo kikatiba.
Alisema NEC inatekeleza mkakati
wa kutoa elimu ya mpiga kura kwa kushiriki kwenye maenesho na mikutano
mbalimbali na imefanikiwa kukutana ana kwa ana na wadau na wananchi.
Aliongeza kuwa kupitia mkakati
huo NEC ilishiriki maonesho ya Sabasaba na Nanenane, mkutano mkuu wa 32
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na kutembelea shule za
Sekondari kwa lengo la kutoa elimu ya mpiga kura.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa ZEC Bw. Salum Kassim Ali. alisema Tume hiyo inaendelea na
marekebisho ya Sheria ya Tume ambayo kupitia mchakato wa marekebisho
hayo imepata uzoefu ambao unaweza kuisaidia tume hizo katika kuboresha
utekelezaji wa majukumu yake.
Alisema pamoja na kufikia hatua
hiyo, ZEC iko kwenye hatua ya mwanzo ya kutoa elimu ya mpiga kura hivyo
uzoefu ulioupata NEC itaisaidia ofisi yake kuboresha utoaji wa elimu ya
mpiga kura kwa upande wa Zanzibar.
Bw. Ali alifafanua kuwa kwa
upande mwingine anaamini NEC itajifunza mengi kutokananna hatua
iliyofikiwa na ZEC katika kufanya marekebisho ya Sheria ya Tume ya
Uchaguzi.
Mkutano huo kati ya NEC na ZEC
unatarajia kutoka na mapendekezo ambayo yanaziunganisha tume hizo katika
kufikia malengo yaliyowekwa kikakitaba.
0 maoni:
Chapisha Maoni