Posted by Esta Malibiche on Oct6.2016 in NEWS
|
Mkuu wa Wilaya ya longido Ndugu Daniel Godfrey Chongolo akishiriki ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi iliyopo wilayani humo. |
|
Ndugu
Daniel Godfrey Chongolo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Longido akiweka Jiwe
kwenye msingi wa nyumba wakati akishiriki Ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi. ....................
Mkuu
wa wilaya ya Longido Bw. Daniel Godfrey Chongolo ameshiriki ujenzi wa
madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi iliyopo wilayani Longido.
Shule hiyo
ambayo ina wanafunzi mpaka wa darasa la tano, ilikuwa na madarasa mawili
tu jambo lililosababisha shughuli za utoaji elimu kwa wanafunzi kuwa
ngumu.
Katika
kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa, Mkuu wa Wilaya akiongozana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Bw. Jumaa Mhina wamefanya
kazi ya ujenzi kwa kushirikiana na wananchi siku nzima ya leo.
Katika hatua
nyingine mkuu huyo wa Wilaya ya Longido aliendesha harambee
iliyofanikisha kupatikana kwa jumla ya shilingi milioni 10.
|
|
Wananchi
wilayani Longido wakiwa katika harakati za Ujenzi wa vyumba viwili vya
Madarasa kwenye shule ya Msingi Lanchi, baada ya kuhamasishwa na mkuu wa
Wilaya hiyo Ndugu Daniel Godfrey Chongolo. |
|
Kazi ya Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Lanchi wilayani Longido ikiendelea.. |
|
Mkuu
wa Wilaya ya Longindo Ndugu Daniel Godfrey Chongolo akiendelea
kushiriki Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi
Lanchi |
0 maoni:
Chapisha Maoni