Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi Kundi la
Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kufungua rasmi kiwanda cha
Usindikaji wa Matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege mkoani Pwani leo
Oktoba 6, 2016
PICHA NA IKULU
…
Na: Frank Shija, MAELEZO
TENESCO
yapewa miezi miwili kuhakikisha inafikisha huduma ya umeme katika
kiwanda cha kusindika matunda na kuzalisha juisi na vinywaji baridi cha
Bakhresa Food Products Ltd kilichopo Mwandege wilayani Mkuranga, Mkoani
Pwani.
Agizo
hilo limetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda hicho
iliyofanyika leo wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.
Amesema
kuwa ni ajabu kwa mwekezaji kuanza ujenzi hadi anamaliza na baadaye
anaanza uzalishaji halafu suala la nishati ya umeme linakuwa kikwazo
hali inayomlazimu mwekezaji kutumia nishati mbadala (Jenereta) kitu
kinachosababisha gharama za uendeshaji kuwa kubwa.
“Ninaagiza
hakikisheni mnafikisha umeme katika kiwanda hiki kabla ya mwezi wa 12,
nia ajabu sana mtu anaanza kujenga mnamuangalia tu, anamaliza
mnamuangalia, Meneja wa TANESCO upo? Hakikisha umeme unafika kama kuna
mtu ana kukwamisha niambie”. Alisema Rais Magufuli.
Aliongeza
ni imani yake kuwa baada ya umeme kufikishwa katika kiwaanda hicho
gharama za undeshaji zitapungua na kupelekea kufanya maboresho ya
maslahi ya wafanyakazi wake.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli ametumia wasaa huo kumuomba Mwenyekiti wa
Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa kuangalia uwezekano wa
kufanya uwekezaji kama huo katika maeneo mengine ya kikanda hili kutoa
fursa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kupata soko la bidhaa
zao.
Kwa
upande wake Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Makampuni ya Bakhresa
unasaidia kuchochea kilimo cha matunda na kutoa fursa ya soko la uhakika
kwa wakulima.
Mwijage
alisema kuwa Sekta ya Viwanda nchini imeendelea kukuwa, aliongeza kuwa
adhima ya kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati kutokana na viwanda
itatimia endapo wafanyabiashara wenye viwanda watakua wazalendo kama
Bakhresa.
Naye
Mwakilishi wa Kampuni ya Bakhresa Food Production Ltd Bw. Yusuph
Bakhresa ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara
wenye viwanda nchini, hali ambayo itasaidia kufikia lengo la Serikali ya
Awamu ya Tano ya kuitaka Tanzania kuwa nchi yenye viwanda ifikapo mwaka
2025.
0 maoni:
Chapisha Maoni