Posted by Esta Malibiche on Oct7.2016 in NEWS
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefunga rasmi Kongamano la 30 la Kimataifa la
Wanasayansi Watafiti lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu (NIMR) lililokuwa la siku tatu Jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri Dk. Kigwangalla amewaeleza wanasayansi hao watafiti kuwa
Serikali inashirikiana nao bega kwa bega katika jukumu la maendeleo hapa
nchini hivyo uwepo wao ni kielelezo tosha cha maendeleo ya Taifa na
watu wake hasa katika Nyanja za kiuchumi, Afya, Mazingira na mambo
mengine ya kimaendeleo.
Aidha,
amebainisha kuwa changamoto za magonjwa ya virusi yanayotokana na Mbu
ambapo ameahidi amewahidi wanasayansi hao na Wizara yake kushirikiana
nao katika kulipitia ufumbuzi.
Dk.Kigwangalla
amewahakikishia Wanasayansi hao kuwa, masuala yote ya kuimalisha
huduma za Maabara katika ngazi za msingi kwani suala hilo amekuwa
akilifanya kila mahala anapokwenda kwenye ziara zake juu ya upatikanaji
wa huduma Maabara bora kwenye sehemu za Afya.
“Nimependa
maombi yenu haya juu ya kuimalisha huduma za Maabara kwenye ngazi za
msingi. Suala hili nimekua nikilifuatilia kila ziara zangu kwenye vituo
vya Afya na Hospitali zote hivyo nitalibeba hili na nitaendelea nalo kwa
sababu nina aamini kutoa huduma za afya bila kuwa na huduma madhubuti
za Maabara ni kuchezea afya za watanzania wenzetu, Ni lazima tuwe na
huduma bora za Maabra zetu na suala hili tutakaa mimi na Mh. Waziri
kuona namna ya kufanyia maboresho zaidi.” Amesema Dk.Kigwangalla.
Aidha, Dk. Kigwangalla aliwatunukia vyeti maalum wanasayansi Vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.
Kongamano
hilo la siku tatu, Oktoba 4-6, awali lilizinduliwa na Makamu wa Rais
Mh. Mama Samia Suluhu Hassan ambaye pia aliwahakikishia Wanasayansi
Watafiti hao kuwa Serikali inatambua mchango wao na wataendelea na
juhudi za kuwalinda kwani ni nguzo muhimu ya kufikia malengo ya
millennia ya ukuaji wa kiuchumi.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela amesema
kufikia tamati ya kongamano hilo ni ishara tosha maandalizi yake
yalikuwa mazuri na washiriki wote walioshiriki wamejifunza mengi huku
wakiwa ni mfano wa kuigwa kwa elimu walioipata hapo.
Nchi
mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika ambapo washiriki zaidi ya 300
wameshiriki huku mada zaidi ya 220 zikiwasilisishwa na kujadiliwa kwa
pamoja na wataalam hao.
Nchi
ambazo zinashiriki kongamano hilo kuwa ni Afrika Kusini, Kenya, Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Australia, Denmark, Ubeljiji,
Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Uswis, Kanada, Sweden, Norway, Marekani,
Bangladesh, Thailand na wenyeji Tanzania.
(Picha zote na Andrew Chale)






0 maoni:
Chapisha Maoni