Ijumaa, 7 Oktoba 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA CZECH ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Posted by Esta Malibiche on Oct7.2016 in NEWS

 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje  Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika
masuala ya usalama kupitia njia za mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu.Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akizungumza na Ujumbe
kutoka Jamhuri ya Czech, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka
Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(wa kwanza kushoto), wakati wa mazungumzo
yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo,
teknolojia na mbinu  za kukabiliana na
uhalifu. Mazungumzo  yalifanyika ofisini
kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe  kutoka  Jeshi la Polisi,Kamishna  Albert Nyamhanga
akijitambulisha kabla ya kuanza mazungumzo kati ya  Wizara ya Mambo ya Nje ya
Jamhuri ya Czech na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala
ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu.Meza kuu ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Hamad Masauni(kushoto) na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek.Mazungumzo  yalifanyika jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka
kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(kushoto),
baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu
kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na
mbinu  za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo
yalifanyika ofisini kwa naibu
waziri,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Pavel
Rezac, akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano
katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana
na uhalifu.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech,
Ivan Jancarek Mazungumzo  yalifanyika
ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.
 
(Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

0 maoni:

Chapisha Maoni