Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Mwigulu acharuka tukio la kupigwa mwanafunzi Mbeya

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba 
Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya walimu wa shule ya Mbeya Day wanaodaiwa kumshushia kipigo mwanafunzi, MKuu wa Shule na baadhi ya walimu wamechukuliwa na polisi kwa mahojiano asubuhi leo.

Hatua hiyo imekuja  baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanafunzi  huyo wa kidato cha tatu, Sebastian Chinguka akipigwa kikatili na walimu.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 28 baada ya mwanafunzi huyo kutofanya zoezi la somo la Kiingereza.  Zinaeleza kuwa walimu waliofanya kitendo hicho walikuwa kwenye mafunzo kwa vitendo.

==>Taarifa rasmi za Waziri wa Mambo ya Ndani

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.

Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian , darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndipo walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga .

Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza  na ndiye  aliyechukua video.

Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.

Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.

MWIGULU Nchemba, W MNN 

0 maoni:

Chapisha Maoni