Posted by Esta Malibiche on Oct6.2016 in SIASA
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (wa tatu kulia), akisaini kitabu
cha wageni baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa BarazaKu Maalumu la Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani
Mwanza, uliofanyika “Gandhi Hall” Jijini Mwanza.
Mongela
amewataka vijana kubuni njia mbalimbali halali za kuwaingizia kipato
ikiwemo ujasiriamali badala ya kukaa bila kazi huku wakijivunia kuwa
kwenye vyama vya siasa.
Amesema
ni vyema wanaoingia kwenye siasa wakahakikisha wana shuguli za kufanya
ambapo amewasihi wajasiriamali wakiwemo Machinga kuwa tayari kufanya
biashara zao katika maeneo yaliyoainishwa na kwamba watakaotii hilo,
watanufaika moja kwa moja na mikopo inayotolewa na halmashauri ya Jiji
la Mwanza.
Naye
Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odila Batimayo, kwa niaba ya umoja
huo, amempongeza Rais John Magufuli kutokana na utendaji wema wa kazi
ikiwemo kuanza kutimiza ahadi zake ndani ya miezi tisa ya uongozi wake
kama vile ununuzi wa ndege, mabehewa, ujenzi wa miundombinu ya barabara
pamoja na mpango wa elimu bure nchini.
Mwenyekiti
wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, amebainisha kwamba lengo la
mkutano huo ni kuyapongeza makundi mbalimbali yakiwemo machinga,
mamantilie na bodaboda kutokana na mchango wao katika kufanikisha
ushindi katika uchaguzi wa mwaka jana, ambapo pamoja na mambo mengine
wajumbe wa mkutano huo wamepata fursa ya kuchangia damu.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (katikati), akisaini kitabu cha
wageni baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa BarazaKu Maalumu la Umoja wa
Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,
uliofanyika “Gandhi Hall” Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela, akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, akizungumza kwenye mkutano huo
Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odila Batimayo, akisoma taarifa ya UVCCM Nyamagana kwenye mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Wajumbe pamoja na Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Taswira
ya mkutano wa Baraza Kuu Maalumu ya UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani
Mwanza, ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya
siku ya kuanzishwa kwa umoja huo, “UVCCM DAY” kitaifa.
Imeandaliwa na BMG
0 maoni:
Chapisha Maoni