KAMPUNI
ya IMPACTAFYA imezindua rasmi program ya Mazoezi Movement to Fitness
kuhamasisha Watanzania kuwa na kaliba ya kufanya mazoezi kuepukana na
matatizo yatokanayo na kutofanya mazoezi.
Akizungumza
na waandishi wa habari, jana Habari Maelezo Mkurugenzi wa IMPACTAFYA,
Bhakti Shah amewataka watanzania kuamka na kulichukulia suala la kufanya
mazoezi kuwa jambo la kupewa kipaumbele.
Alisema
Tanzania iko hatarini kupoteza mamillioni ya watu ambao ni nguvu kazi
ya jamii kwa kutofanya mazoezi, “Ugonjwa wa kisukari ambao kwa kawaida
huwapata watu wazima unaongezeka kwa haraka ulimwenguni pote na sasa
hata vijana wapo hatarini kwa sababu hawafanyi mazoezi, asilimia 20 hivi
ya vifo vyote vilivyotokea miongoni mwa watu walio na umri wa miaka 21
hadi 45, vilisababishwa na kukosa kufanya mazoezi.”
Alihoji
kama Teknolojia Ni Baraka au Laana? Bhakti alisema “Leo watu wana afya
bora na wanaishi muda mrefu zaidi kuliko wale walioishi karne nyingi
zilizopita kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ambayo imekuja na
Vifaa vya kisasa vya matibabu, lakini ni teknolojia hiyo hiyo iliyoleta
mashine ambazo zimesaidia kupunguza kazi nyingi ngumu na hivyo watu
wengi waishi maisha ya kukaa tu bila kufanya mazoezi yakutosha.” alisema
“Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni yenye kichwa cha habari International Cardiovascular Disease Statistics, Shirika
la Moyo la Marekani lilieleza kwamba “mabadiliko ya kiuchumi, watu
kuhamia mijini, usitawi wa viwanda, na kuenea kwa biashara za kimataifa,
na mitandao ya kijamii, imesababisha kuleta mabadiliko katika mitindo
ya maisha ambayo huchangia ugonjwa wa moyo.” Ripoti hiyo inataja
“kutofanya mazoezi na kula vyakula visivyofaa” kuwa mambo yanayochangia
sana ugonjwa huo.
Alisema
Mtindo wa maisha wa Leo wa mijini, mfanyakazi anaweza kuketi mbele ya
kompyuta karibu siku nzima, aende mahali popote atakapo kwa gari lake,
na atazame televisheni na kubrows kwenye mitandao ya kijamii jioni yote,
na hivyo kujiingiza katika maradhi ambayo yamehatarisha maisha.
“Watu
wengi zaidi wanapendelea kutumia motokaa na pikipiki badala ya
baiskeli, asilimia 25 ya safari zote hazizidi kilometa moja hivi,
asilimia 75 ya safari nyingi fupi hufanywa kwa gari. Hii ni hatari”
alisema.
Alisema,
Teknolojia ya kisasa pia imefanya watoto wakae tu bila kufanya mazoezi
ya kutosha. Uchunguzi mmoja ulioonyesha kwamba kadiri michezo ya video
inavyozidi kuwa yenye kufurahisha na halisi, ndivyo watoto wanavyotumia
wakati mwingi zaidi kutazama televisheni na vitumbuizo vingine ambavyo
huwafanya watoto hao wakae tu bila kufanya mazoezi ya kutosha.
Akiongela
hatari za kukaa tu bila kufanya Mazoezi ya kutosha alisema watu wengi
wanapatwa na matatizo ya kimwili, kiakili, na kihisia. Akitolea mfano,
hivi karibuni shirika moja la afya nchini Uingereza liliripoti kuwa
“Watoto wasiofanya mazoezi wanaweza kukabili hatari ya kutojiheshimu,
kuwa na wasiwasi mwingi na mifadhaiko mingi.
Ripoti
hiyo ilisema kuna uwezekano mkubwa kwamba watoto hao watavuta sigara na
kutumia dawa za kulevya kuliko watoto wanaofanya mazoezi.
Bhaktti
alieleza kuwa Watu wengi hupatwa na shinikizo kubwa la damu, kiharusi
na ugonjwa wa moyo, aina fulani za kansa, ugonjwa wa mifupa, na
uwezekano mkubwa wa kuwa wanene kupita kiasi kwa kula vyakula vyenye
kalori nyingi na kutofanya mazoezi.
“Swala
la kutofanya mazoezi ni TIME BOOM . Matatizo na madhara yatokanayo na
kutofanya mazoezi ni ya Ulimwenguni Pote, ni wakati sasa Tanzania
Kuamka. Tunayaita mashirika, makampuni na watu binafsi kuungana nasi
katika MOVEMENT TO FITNESS kuliokoa taifa hili.
Alisema
tayari zipo Nchi nyingi sasa zinazoendesha kampeni zao za Kitaifa za
kufanya mazoezi kama vile Mexico, Brazili, Jamaika, New Zealand,
Finland, Shirikisho la Urusi, Morocco, Vietnam, Afrika Kusini, na
Slovenia. inafaa kwa Tanzania kuwa na wasiwasi kuhusu hali ilivyo sasa.
“Ingawa
hatari za kutofanya mazoezi kabisa zimezungumziwa sana, sisi tunasema
si lazima uwe na membership card ya gharama kubwa kuwa na afya bora.
Unaweza kutembe na kukumbia na ratiba nzuri ya kufanya mazoezi hayo”
alisema.
“Kuendesha
kampeni yetu tumewateua machampion wetu “Shamim Mwasha, mmiliki wa blog
ya jamii 8020fashions na Monica Joseph, Mon Finance pamoja na wengine
akiwemo msanii Manyolee ambaye ametunga na kuimba wimbo wakwanza
Tanzania kuhamashisha ufanyaji wa mazoezi.”
“Kupitia
Movement to fitness tuna kipengele cha Fun run walk ambayo yakwanza
ilifanyika mwezi uliopita wa september, fun run walk nyingine inafuata
mwezi huu wa kumi, tarehe 8 siku ya jumaamosi pale Golden tulip
oysterbay kuanzia saa 10 hadi saa 1 usiku, ambapo tutatoa mbinu
mbalimbali za kuwa fit kiakili na kimwili. Tunawakaribisha kujiunga nasi
kwa kujiandikisha kupitia no ya simu 0754 694643 au email move@impactafya.com
“Kila
mmoja wetu ana daraka la kutunza afya yake mwenyewe. Jiulize, ‘je
nimefanya mazoezi ya kutosha? Ikiwa sivyo, ninaweza kufanya nini ili
niongeze mazoezi yangu?’ unaweza kuwasiliana nasi na kujiunga na
Movement to Fitness ambayo inasimamia na kufuatilia mwendo wako mzima wa
kuishi kama mwanamazoezi.
________
Bhati Shah
Managing Director – IMPACTAFYA
0 maoni:
Chapisha Maoni