Posted by Esta Malibiche on Oct5.2016 in NEWS
Naibu Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula ametembelea
Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kukutana na Waziri Mh. Ummy
Mwalimu pamoja na Makatibu wa Wizara hiyo.
Dk. Zainabu Chaula ametembelea Wizara hiyo
hii ni baada ya kuapishwa rasmi na Ikulu Jijini Dar e Salaam na Rais Dk. John
Pombe Magufuli, Septemba 26.2016.
Akiwa Wizarani hapo amepata kufanya
mazungumzo ya kiutendaji kwa pamoja akiwemo Waziri Afya na Makatibu wake.
Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki
Ulisubisya alipomtembelea ofisini kwake Wizarani jana Oktoba 4.2016.






0 maoni:
Chapisha Maoni