Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (kulia) akizungumza na wananchi wa mji wa Misungwi kuhusu
masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo hilo. Katika hotuba yake,
Kitwanga aliwaka wananchi hao kufanyakazi ili jimbo hilo lizidi kusonga
mbele. Pia Mbunge huyo alipiga marufuku uchezaji wa pool table wakati wa
kazi.
Mkazi wa Misungwi mjini, Songoro
Msafiri (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (kulia aliyekaa), mara baada ya Mbunge huyo kumaliza kuzungumza
na wananchi hao na kuruhusu kuuliuzwa maswali mbalimbali yanayowakera
jimboni humo. Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili
waliletee maendeleo jimbo lao.
Wananchi wa mjini Misungwi
wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga katika mkutano wa
hadhara uliofanyika mjini huo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akizungumza na mabalozi wa mashina wa CCM katika Ukumbi wa
Mikutano wa CCM Wilaya ya Misungwi. Kitwanga aliwashukuru mabalozi hao
kwa kumchagua na kuwaomba washirikiane zaidi ili kuliletea maendeleo
jimbo hilo. Picha zote na Felix Mwagara.
……………………………………………………………………………………………
Na Felix Mwagara, Misungwi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani Misungwi kuwakamata vijana
watakaocheza mchezo wa pool wakati wa kazi jimboni humo.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara uliofanyika mjini Misungwi na kuhudhuria na mamia ya wananchi wa
mji huo, Kitwanga alisema wilaya hiyo inahitaji maendeleo na mabadiliko
makubwa zaidi na mabadiliko hayo yanakuja kutokana na ufanyaji kazi.
Aliserma kazi ndio msingi wa maendeleo hivyo ili maendeleo yapatikane
lazima watu wafanyekazi katika maeneo yao.
“OCD (Mkuu wa Jeshi la Polisi
Wilaya) nisione na sitaki kusikia vijana wa Misungwi wanacheza pool
asubuhi, nashangaa sana kwanini mnapenda pool, pool sio kazi, na
maendeleo hayawezi yakaja kwa kucheza pool, chezeni jioni baada ya muda
wa kazi,” alisema Kitwanga
Kitwanga aliwataka wananchi
jimboni kwake kuanzisha vikundi ili waweze kupewa mikopo kupitia fedha
alizoziahidi Rais John Magufuli kuwa atatoa kwa kila kijiji shilingi
milioni hamsini.
“Fedha zipo jirani kuja, hivyo
anzisheni vikundi ili muweze kukopeshwa fedha hizo na muweze kufanya
mambo ya maendeleo, fedha hizo ni kwa ajili ya mikopo hivyo tumieni
fursa hiyo kwa kuanzisha vikundi vyenu ili muweze kuzipata fedha hizo
kwa uharaka zaidi,” alisema Kitwanga.
Wakati huo huo, Mbunge huyo
alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kuhakikisha
anawachukulia hatua kali wauguzi na madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya
Misungwi watakaoomba rushwa kwa wagonjwa au ndugu wa wagonjwa. Kitwanga
alisema hayo baada ya kulalamikiwa kwa muda mrefu kukithiri kwa rushwa
katika hospitali hiyo ya wilaya.
Hata hivyo, Waziri Kitwanga
aliwahakikishia wananchi wa jimbo hilo wawe watulivu na wasubiri
maendeleo, na pia waendelea kuchangia maendeleo ya jimbo lao ikiwemo
uchangiaji wa madawati katika shule zao. Kuhusu barabara Kitwanga
alisema barabara zote ambazo hazipitiki zitatengenezwa hivi karibuni na
tatizo la maji litakuwa historia kwani mipango ya upatikanaji wa maji
hayo ilishakamilika.






0 maoni:
Chapisha Maoni