Ndugu
zangu waandishi wa habari, kwanza niwashukuru kwa ushirikiano ambao
mmeendelea kutupatia, pia niwashukuru wananchi wote kwa ujumla kwa
ushirikiano wao wa kudumisha amani na usalama hapa nchini. Tumewaiteni
hapa leo kuzungumzia matukio ya ubakaji
Katika siku za hivi karibuni,
Matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo yamekuwa yakiongezeka kwa
kiwango kikubwa, ongezeko hili limebainika kutokana na ufuatiliaji
tulioufanya kupitia matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi
ambapo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2016 kumeripotiwa
matukio 1765 ukilinganisha na matukio 1585 katika kipindi kama hicho
mwaka 2015 ikiwa ni ongezeko la matukio 180.
Katika matukio ya Januari hadi
machi 2016, jumla ya watuhumiwa 823 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani
ingawa bado kumekuwa na tabia ya wazazi na walezi kuficha watuhumiwa wa
ubakaji na kumaliza kesi hizo kirafiki au kifamilia jambo ambalo ni
kinyume cha sheria bila kuzingatia madhara aliyoyapata mtoto.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la
Polisi nchini linakemea vikali wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo
viovu vya ubakaji na wazazi ama walezi wanaofumbia macho vitendo hivyo
na kuingia makubalino na watuhumiwa kwa kupeana fedha kama fidia ili
wamalize kesi kiundugu au kifamilia.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa
Wazazi, walezi, Viongozi wa dini, Asasi za kiraia, walimu na Wananchi
kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano katika kushughulikia vitendo
hivyo ikiwemo kuwafichua wazazi au walezi wanaofanya makubaliano ya
kumaliza kesi za ubakaji kirafiki au kifamilia ili kukomesha vitendo
hivyo.
Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
0 maoni:
Chapisha Maoni