Mganga Mkuu wa mkoa wa Njombe
Dokta Samuel Mgema akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma za
madaktari bingwa mjini Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu
wagonjwa mbalimbali kwa mikoa husika, kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali
Profesa Mohammed Bakari
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na
Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa mjini
Njombe wanaowafanyia upasuaji na matibabu wagonjwa mbalimbali kwa
mikoa husika,kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed
Bakari.
Baadhi ya watumishi na madaktari pamoja na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Mkuu wa mkoa wa NJOMBE Mh.
Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja viongozi mbalimbali mara
baada ya uzunduzi huo uliofanyika mjini Njombe leo.
………………………………………………………………………………………………..
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirkiana na Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya, wiki hii inaendesha zoezi la huduma za madaktari bingwa katika
mikoa ya Njombe na Iringa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa zoezi hilo mkoani Njombe Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohammed
Bakari amesema serikali itaendelea kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapelekwa katika maeneo
mengi ambako wananchi wanahitaji huduma za madaktari bingwa ili
kukabiliana na upungufu uliopo.
Amesema pamoja na kuendelea
kutumia huduma hizo za muda za madaktari Bingwa, Serikali kupitia Wizara
ya Afya, itajitahidi kujenga miundo mbinu bora ya sekta ya afya na
kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi walio wengi.
Akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mganga Mkuu wa Serikali, Mganga Mkuu wa mkoa wa Njombe
Dokta Samuel Mgema, amesema hospitali yake inakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo na ufinyu wa nafasi
ikilingwanishwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohudumiwa katika
hospitali hiyo.
Ameomba Serikali iharakishe
mchakato wa kujenga Hospitali mpya ya mkoa ili kukidhi mahitaji ya
wananchi wa mkoa wa Njomba, kwani hospitali inayotumika hivi sasa ya
Kibena ilikuwa na hadhi ya hospitali ya wilaya na kupandishwa hadi baada
ya kutangazwa kwa mkoa mpya wa Njombe, miaka minne iliyipita.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za
Tiba na Ushauri wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dokta Frank Lekey
amesema huduma hizo za madaktari bingwa zimekuwa zikitolewa na Mfuko
wake kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya kupeleka huduma
bora za matibabu kwa wanachama wa NHIF na kwa wananchi kwa ujumla.
Asema hadi sasa huduma hizo
zimeshatolewa katika mikoa 14, ambazo zaidi ya wagonjwa 11,400
wamepatiwa huduma, miongoni mwao zaidi ya wagonjwa 340 walifanyiwa
upasuaji wa kitaalamu.
Amesisitiza kuwa huduma hizo
zinatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi kwa kufuata taratibu za
kawaida za malipo za hospitali husika.
0 maoni:
Chapisha Maoni