Ijumaa, 22 Aprili 2016

Kasi ya MAGUFULI yawagusa wengi,SHEIKH JALALA amfananisha na mwanafunzi huyu wa Mtume


Kiongozi Mkuu wa chuo cha kiislam HAWZA Imam Swadiq ambaye  pia ni kiongozi mkuu wa waislam wa dhehebu la Shia Ithnasheria nchini Tanzania SHEKH HEMED JALALA akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam
 Na Exaud Mtei
Watanzania wametakiwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DR JOHN POMBE MAGUFULI za kupambana na ufisadi na kuleta Amani na usawa katika nchi kwani ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote duniani.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam mchana wa leo kiongozi Mkuu wa chuo cha kiislam HAWZA Imam Swadiq ambaye  pia ni kiongozi mkuu wa waislam wa dhehebu la Shia Ithnasheria nchini Tanzania SHEIKH HEMED JALALA wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa  mmoja kati ya wanafuzi wa mtume ambaye ni  Imam Ali aliyekuwa kiongozi jasiri kati ya wanafunzi wa mtume Mohamad amesema kuwa Rais Magufuli ameonyesha njia ambayo Tanzania inatakiwa kuelekea hivyo ni wakati wa watanzania kuunga mkono juhudi hizo.
Amesema kuwa Imam Ali ambaye wanaadhimisha kuzaliwa kwake Zaidi ya miaka 1430 Alikuwa ni kiongozi aliyepigana kuleta usawa kwa watu wote pasipo kujadi dini zao,alipinga ufisadi,uadilifu,jambo ambalo amesema linafanana na analolifanya Rais wa Tanzania kwa sasa hivyo ni wakati wa kumuunga mkono.



“Naweza kumfananisha Rais wetu na kiongozi huyu Iman Ali na serikali aliyokuwa anaiongozi japo siwezi kusema wanafanana kwa asilimia ngapi ila mambo anayoyafanya Rais Magufuli ndiyo yale yale aliyoyafanya Imam Ali wakati akiongoza serikali”.amesema kiongozi huyo
Aidha ameongeza kuwa katika utawala wa Imam Ali ulisimamia sana katika kuondoa ujinga huku ukiamini kuwa ili nchi ipate maendeleo ni lazima kufuta ujinga na kuwapa watu Elimu jambo ambalo Rais Magufuli limekuwa kipaumbele chake hadi kuweka elimu bure nchini ambapo amesema kuwa ni njia moja wapo kubwa na nzuri ya kuyafikia maendeleo ya taifa.

Shekh JALALA amemaliza kwa kwa kuwataka watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini kuhakikisha wamamwombe sana Rais wa Tanzania ili aweza kufanikisha lengo lake la kuifikisha Tanzania katika mafanikio ya kimaendeleo

0 maoni:

Chapisha Maoni