Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Issa Hayatou
amemtumia salamu za pongezi Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa kuwa
Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) mwishoni mwa juma lililomalizika.
Katika
salamu zake, Hayatou amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya Utendaji na
yeye binafsi wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira
wa Miguu Zanzibar (ZFA).
CAF wanaimani na uzoefu wa Ravia katika uongozi, kuwa ataendeleza uongozi bora kwa faida ya maendeleo ya soka visiwani Zanzibar.
Aidha Hayatou amewatumia pia salamu za pongezi, Mzee Zam Ali na Ali Mohamed kwa kuchgauliwa kuwa makamu wapya wa Rais wa ZFA.
Hayatou
amewatakia mafanikio mema katika nafasi mpya hizo walizochaguliwa na
kuahidi CAF itaendelea kuwapa ushirikiano wa maendeleo ya mpira wa miguu
visiwani Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni