Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam jioni hii, akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia)
pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana
Pallangyo.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa
wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda
mpaka Jijini Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini
Kampala. Mbali na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia),
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo
(wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James
Mataragio walipokuwa wakimsubiria Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo alierejea jijini Dar es salaam leo akitokea Jijini
Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi
Tanga.
0 maoni:
Chapisha Maoni