Na Masanja Mabula –Pemba
JESHI la Polisi Mkoa
wa Kaskazini Pemba limeagiza kukamatwa na kufikishwa
mahamakani aliyekuwa , Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni (CUF) kwa mihula
miwili (2005-2015) Subeti Khamis Faki anayetuhumiwa kutenda kosa la
shambulio la kuumiza mwili .
Kamandawa Polisi Mkoa wa
Kaskazini Pemba , Kamishina Msaidizi Mwandamizi Hassan Nassir Ali
akizungumza na mwananachi Ofisini jana , alisema kwamba Subeti
anatuhumiwa kumshambulia kwa kumpiga magongo Mbwana Nassor Shilingi (30)
na kumsababishia maumivu mwilini .
Alisema kuwa tukio hilo
limetokea jana (juzi) aprili 20 majira ya saa 2:15 asubuhi huko Shehia
ya Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni baada ya kutokea hali ya kutoelewana
kati ya pande hizo mbili .
Kamanda Hassan Nassir Ali
alizidi kufahamisha kwamba siku ya tukio huko Mjini Wingwi Subeti
alimwita mbwa , kijana huyo wakati akimzuia kuchota maji kwenye bomba ya
maji nyumbani kwa Mbwana Nassor Shilingi.
“Nimemwagiza OCD Wilaya ya
Micheweni amkamate na kumfikisha mahakamani aliyekuwa mwakilishi wa
Jimbo la Micheweni , Subeti Khamis Faki kutokana na kutenda kosa la
shambulio ya kuumiza mwili ”alifahamisha .
Aidha taarifa zaidi zinasema
kwamba ugomvi umetokea wakati Subeti akijaribu kumzuia jirani yake
kutotumia bomba ya maji inayomilikiwa na ndg Mbwana akidai kwamba vitu
vya wanachama wa CCM wamegoma kuvitumia .
Hata hivyo kamanda Nassir akikataa kulihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa kwani alisema kwamba ni ugomvi wa watu binafsi .
Akizungumza na mwananchi
mjeruhiwa wa tukio hilo alisema kuwa chanzo chake kimesababishwa na
mgeni aliyekuja katika mtaa wao , ambapo alikwenda kwenye bomba ya maji
kwa ajili ya kufua nguo zake na ndipo Subeti alimwambia asitumie vitu
vya mbwa kwani wamevigomea .
Alieleza kwamba baada ya maneno
hayo , mjeruhiwa katika tukio hilo alipinga kuitwa mbwa na wakati
akiondoka kwenye bomba hiyo alijikuta akipigwa magongo sehemu za
mgongoni na kupata maumivu .
“Unajua alikuja mgeni hapa
mtaani petu , sijui kama ni CCM au CUF akaanza kufua nguo katika bomba
ya maji , lakini cha kushangaza Subeti alimkataza kutumia bomba hii
akisema ni ya mbwa na sisi tumewagomea ”alieleza Mbwana .
Baada ya kutokea kwa tukio hilo
, mtuhumiwa huyo alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kuzungumzia
tuhuma hizo alidai kutokuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari kwa
wakati ule .
Kumekuwako na matukio ya
kushambuliana mara kwa mara katika shehia ya Mjini Wingwi baada ya
kufanyika uchaguzi Mkuu wa marejeo hapo machi 20 uliokipa ushind chama
cha CCM .
Awali tukio kama hilo lilitokea
baada ya Tume ya Uhaguzi kutangaza matokeo ya uchaguzi huo ambapo fujo
zilotokea na kusababisha askari kutumia mabomu ya kutoa machozi
kuwatuliza wafuasi wa vyma vya CCM na CUF walikuwa wakishambuliana .
0 maoni:
Chapisha Maoni