Vijana
wametakiwa kugeuza changamoto kuwa fursa na kuwa na utamaduni wa
kujiajiri na kuchapakazi kwa bidii badala ya kusubiria kuajiriwa huku
wakilaumu mamlaka zinazoshughulika na vijana nchini.
Hayo
yamesemwana Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua mdahalo wa siku mbili
kujadili hatma ya ajira kwa vijana Tanzania uliyoandaliwa na Shirika la
Kimataifa la Ajira (ILO) jana jijjni Dar es Salaam.
“Changamoto
ya ukosefu wa ajira inaweza kutumika kama fursa kwa kijana
anayejitambua kwakuwa na fikra chanya itakayomuwezesha kutumia elimu
aliyoipata kujiajiri bila kuona aibu kufanya baadhi ya kazi mbali ya
kuwa amesoma hadi elimu ya juu hivyo kujiongezea kipato,”alisema Prof.
Gabriel.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi
ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bi. Mary Kawar amesema
kuwa shirika hilo liko tayari kuwajengea uwezo vijana katika masuala ya
ajira ili kupunguza tatizo la ukosefuwaajira kwa vijana.
Naye
mshiriki wa mdahalo huo Bw. Masson Kimbo ameiomba serikali kupitia
mifumo ya elimu nchini itakayowawezesha vijana kujengewa uwezo wa
kujiajiri na kuwa na fikra pana katika masuala ya ujasiriamali.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akifungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania
ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha
vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani
Mkurugenzi
Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya,
Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar akizungumza na vijana (hawapo
pichani) wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania
ulioandaliwa na shirikila
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (kushoto) akitoa mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa
vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO)
na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa
la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi.
Mary Kawar baada ya kufungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa
Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na
kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani






0 maoni:
Chapisha Maoni