Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa
viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama
chama ambao ni Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa
Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na
Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa
Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa
katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi
mbele ya waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam,
Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi
kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum
Makunganya aliyehamia chama hicho.
…………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa
Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa
mikoa ya Mtwara na Dar es
Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).
Viongozi waliokihama chama hicho ni Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na
Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu,
Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga
CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa
habari.
Wenyeviti
hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa
CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza
rasmi kuwa wanachama wa chama hicho.
Makunganya
alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba
1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi
ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.
Wakizungumzia
sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho
kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita
viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri
Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.
Walisema
sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama
hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali
ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .
“Nyie
waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa
Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es
Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama
vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa
uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.
Muabhi
akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK
inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya
chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea
misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Muabhi
aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa
kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki
wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea
Bungeni.
“Serikali
ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja
gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni,
wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao
serikalini,”alisema.
Mwenyekiti
wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya
ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi
kutoka kwao.
0 maoni:
Chapisha Maoni