Wanamuziki
wa dansi, taarab, bongo fleva na wadau wa muziki waishio Dar es Salaam,
Alhamisi hii watakutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa
Paul Makonda ili kubadilisha mawazo juu mwenendo wa kazi zao.
Wasanii na wadau hao watakutana
na Makonda ndani ya ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni kuanzia saa
5asubuhikatika mkutano utakaohudhuriwa pia na wamiliki wa kumbi za
starehe wa mkoa wa Dar es Salaam.
Mkutano huo umeandaliwa na kamati
ya ushirikiano ya wanamuziki wa dansi, taarab na wamiliki wa kumbi za
starehe iliyoundwa hivi karibuni ili kujadili kwa undani changamoto za
sheria ya biashara ya vileo na burudani ambazo ziko tangu mwaka 1968 na
1972.
Mmoja wa wasemaji wa umoja huo wa
wanamuziki wa dansi, taarab na wamiliki wa kumbi za starehe, Juma
Mbizo, ameuambia mtandao huu kuwa maombi yao ya kumwalika Mkuu wa Mkoa
katika mkutano huo, yameshawasilishwa kwa Mkuu huyo wa Mkoa.
Jumba Mbizo amewataka wanamuziki,
wadau wa muziki na wamiliki wa kumbi za starehe watakaopata taarifa za
mkutano huo kwa njia yoyote ile, wafike kwa wingi Vijana Social.
Mbizo amesema mkutano
huohauhusiani na chama chochote cha muziki, bali umeandaliwa na
waathirika wakuu sheria hizo za burudani na vileo ambao ni wanamuziki na
wamiliki wa kumbi za starehe.
0 maoni:
Chapisha Maoni