Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr Joyce Ndalichako amewataka wadhibiti ubora wa Elimu nchini kuhakikisha wanatoa tarifa za utoro wa walimu
katika ngazi za juu iili wizara husika
iweze kuwachukulia hatua
Waziri Ndalichako aliitoa kauli hiyo jana
wakati alifungua mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyo
fanyika katika chuo cha walimu Kleruu mkoani hapa yaliojumuisha mikoa sita ya
nyanda za juu kusini ambayo Iringa,
Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya. Mafunzo hayo yana husu
uhakiki wa ubora wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu).
Akifungua mafunzo hayo Dr Ndalichako alisema
serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Dr.John Magufuli imepania kukuza ubora wa elimu inayo tolewa hapa nchini hivyo lazima iboreshwaili
kiwango cha ufauru kiweze kuongezeka
Kumekuwa na changamoto kubwa
mashuleni katika usahihihi wa takwimu
kutokana na uzembe wa baadhi ya wathibiti kutoa taarifa za uongo kuhusu idadi ya walimu wanaohudhuria vipindi
kufundisha pamoja na wanafunzi wanaohudhuria masomo
Ndalichako alisema wakaguzi wanapaswa
kuhakiki mitaala inayotolewa kama inafundishwa ipasavyo pamoja na kukagua
mahudhurio ya walimu na wananfunzi ili kupata uwiano na pale inapobainika kuwa
kuna mapungufu taarifa itolewe mapema ili kuweza kutatua tatizo kabla ya athali haijatokea.
Tumeshuhudia idadi kubwa ya wafanyakazi hewa nchini na
sekta ya inayooongoza ni hii ya Elimu,hivyo hatuna budi kuwa waangalifu katika
utumishi wetu kutokanan na dhamana tuliyopewa na kiongozi wetu.Sitamfumbia
macho kiongozi yeyote katika sekta yangu atakaeleta uzembe kazini nitapambana nae <<<alisema
Alisema swala la uwiano baina ya walimu
na wanafunzi ni muhimu sana ili wanafunzi waweze kufundishwa vzuri na hatimae
waweze kufauhuru kwa kiwango cha hali ya juu.
Alisema eneo lingine ambalo mkaguzi anapaswa kufanya pale
anapokuwa anafanya ukaguzi shuleni anatakiwa kuangalia ubora wa vitabu vinavyotumikapamoja
na vifaa vyote ni lazima viowe na ubora unaosadikiwa kufuata mitaala.
Aidhaaliwataka maafisa Elimu kkuendelea
kutoa Elimu kwa wazazi na walezi kuhusu utoaji wa Elimu bila malipo kutokanan
na baadhi ya wazazi kutokuwa na uelewa wa kutosha kwa kufukiri michango yote
imesitishwa hata wanashindwa kuwanunulia watoto wao mahitaji muhimu ya shule
kama sale na daftari wakitegemea serikali huku wakifikiri serikali ndiyo yenye
mamlaka.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alimuomba waziri kuhakiksha Wahakiki ubora
wanapewa kipaumbele katika kukuza elimu Tanzania kwa kuboreshewa maslai yao ili
waweze kufanya kazi kwa ufanisi
Masenza alisema kuwa wakati serikali
inaendelea kuboresha masalahi ya walimu izingatie sana katika kuhakikisha
nyumba na malimbikizo ya madai yao yanatatuliwa haraka iwezekananyo.Na
alimuomba waziri Ndalichako ku;lisimamia na kuhakikissha linapewa kipaumbele
Naye Mkuu wa wilaya bwana Richard Kasesela akitoa salamu alisema wakati muafaka umefika wa kubadili KKK iliyopo iliyozoeleka sasa yaani
KULA, KULALA na KUCHEZA kuiirejesha kwenye maana halisi ya KUSOMA, KUANDIKA na
KUHESABU kutokana na baadhi ya wanafunzi kuhitimu elimu ya msingi bila kujua
kusoma na kuandika.
Alisema hali hii inatokana na walimu kutofuatilia
maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja pamoja na wazazi kutokuwa makini na watoto
wao kwa kukagua daftari na kutofuatilia masomo yao,na hatimae kuwaachia walimu
pekee.
0 maoni:
Chapisha Maoni