Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Boniventura Mushongi akizungumza na waandishi wa habari kuhusina na
tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Afisa Tarafa wa Kibiti
kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya
Kitunda.(Picha na Victor Masangu)
………………………………………………………………………………………………………….
NA VICTOR MASANGU, PWANI
JESHI la polisi Mkoa wa Pwani
limemkamata na kumfikisha mahakamani Afisa Tarafa wa Kibiti Wilaya ya
Rufiji Mkoani Pwani Selemani Mpangile almaarufu babu konyeza kwa tuhuma
za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita
katika shule ya msingi kitunda.
katika shule ya msingi kitunda.
Akizungumza na Mwandishi wa
habari hizi ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura
Mushogi amesema kwamba tukio hili limetokea juzi majira ya saa 10 jioni
ambapo mtuhumiwa aliamua kutenda kosa hilo kinyume na sheria na
taratibu za nchi.
Mushongi alisema kwamba jeshi
la polisi litaendelea kuvalia njuga vitendo vya ubakaji kwa watoto
wadogo kwani kunaweza kuwasababishia madhara makubwa watoto hao kutokana
na kufanyiwa vitendo kama hivyo wakiwa na umri mdogo.
Kamanda Mushongi amefafanua
kuwa tukio hilo la ubakaji mtuhumiwa alilifanya katika ofisi yake wakati
mwanafunzi huyo alipokuwa akipita nje ya jengo hilo na ndipo alipomwita
na kuingia ndani ambapo alimziba mdomo wake kwa koti leke ili asipige
kelele kasha kutekeleza azma yake ya kumbaka .
Katika hatua nyingene Kamanda
ametoa onyo kwa wanafunzi kuachana na tabaia ya kuwa na tamaa ya
kupenda vitu vya bure, na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha
wanawatunza na kuwalea watoto wao katika misingi mizuri ya kimaadili na
sio kuwa na fikra potofu.
“mimi napenda kutoa onyo kwa
wanafunzi na watoto waache kabisa tabia ya kuwa na tama, kwani wakifanya
hivyo matokeo yake ndio hayo kwani wakati mwingine wanapenda vitu vya
bura kama pipi, soda kwa hivyo hii ni hatari sana, pia na wazazi
wahakikishe wanawalinda watoto wao,” alisema Mushongi.
MATUKIO ya vitendo vya ubakaji
kwa watoto wadogo katika Mkoa wa Pwani bado yanaonekana kuwa ni tatizo
kubwa hivyo kunahitajika juhudi za makusudi zifanyike na serikali katika
kuwachukulia hatua kali za kisheria na kutoa adhabu kali kwa wale wote
watanaobainika kuhusika katika matukio kama hayo.
0 maoni:
Chapisha Maoni