Polisi nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni.
Watu
Zaidi ya mia mbili na hamsini wamekamatwa baada ya maduka mengi
yanayomilikiwa na wanyaruanda kuvamiwa.Uvamizi huo ulitokea baada ya
wanyaruanda kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja.
o Padre
Charles Chilinda ameiambia BBC kuwa kanisa lake linafanya jitihada zote
ili kuweza kuwasaidia wahanga ambao wamekwenda kuomba hifadhi kanisani.
"Kitu
ambacho tunaweza kuwapa ni kwamba watakuwa na usalama wa kutosha kuwa
hapo,tutaenda kuwaangalia na kuwaeleza kuwa hawa sio wazambia ambao
wanagombana nao.hali hii haikubaliki ,kila mtu aliyepo katika ardhi ya
Zambia analindwa na katiba ya Zambia.Ni jukumu letu kudumisha Amani na
tushirikiane katika kulitokomeza hili"
|
0 maoni:
Chapisha Maoni