Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Songwe, Juliana Shonza, akiwa amebebwa na Wanawake, Wajumbe wa Baraza la
Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Momba mkoani hapa jana
alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua
katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Picha na Mpigapicha Wetu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Songwe, Juliana Shonza, akizungumza na wanawake, Wajumbe wa Baraza la
Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe,
jana alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa
kumchagua kwake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Picha na Mpigapicha
Wetu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Iringa, Rose Tweve (kulia) akimsisitiza jambo Mbunge mwenzie wa Mkoa wa
Songwe, Juliana Shonza jana wakati Shonza alipokutana na Wajumbe wa
Baraza la Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Momba mjini Tunduma kwa
lengo la kuwashukuru wajumbe hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa viti
maalum mkoani hapa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Picha na
Mpigapicha Wetu.
Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa
Songwe, Juliana Sonza na Mbunge mwenzia wa Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (
wa tatu kushoto) wakiserebuka na wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CCM
Wilaya ya Momba (UWT) Mkoa wa Songwe, jana walipokutana nao mjini
Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa
mwaka jana kupitia UWT. Picha na Mpigapicha Wetu.
Mbunge
wa Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Sonza (aliyeshika kipaza
sauti) na Mbunge mwenzia wa Mkoa wa Iringa, Rose Tweve ( wa tatu
kushoto) wakiserebuka na wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CCM Wilaya ya
Momba (UWT) Mkoa wa Songwe, jana walipokutana nao mjini Tunduma kwa
lengo la kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana
kupitia UWT. Picha na Mpigapicha Wetu.
…………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Tunduma. Mbunge wa Viti Maalumu
Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza amesema amejipanga vilivyo kuhakikisha
anawainua wanawake wa mkoa huo, kiuchumi kwa kuwazesha kufanya
ujasiriamali utakaowaingizia kipato.
Shonza alitoa kauli hiyo jana
kwa wajumbe wa Baraza la Wawanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT)
Wilaya ya Momba, alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru
kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Shonza ambaye aliongozana na
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve, alisema katika
kuhakikisha adhima yake ya kuwanua wanawake hao inatimia ameanzisha
mfuko maalumu alioita ‘Songwe Women Foundation” utakaolenga kuwasaidia
wanawake wa umoja huo.
“Ninawaombeni sana undeni
vikundi, hakikisheni mnavisajili na fedha ya kusajili vikundi vyenu
nitatoa mimi, na nimeanzia mfuko maalum kwa ajili ya wanawake wote wa
mkoa wa Songwe, na nimeweka Sh 20 milioni na kila kikundi kwenye kata
zenu mtapewa Sh200,000 kwa ajili ya kuanzisha mradi mtakaona unafaa.
Niliwaahidi kuwainua nitafanye mtakavyotaka nyinyi.
Kupitia mfuko huo, nitataka
mniambie ni mradi gani mnataka kuufanya. Lakini mbali na kuwawezesha
kifedha lakini kabla ya kuanza kuanzisha mradi huo kwanza nitawaletea
wataalamu wa masomo ya ujasiriamali watawafundisha ili iwasaidie
kuendesha mradi wenu,” alisema Shonza.
Alisema kupitia mfuko huo, tayari
ameanza kuzungumza na wadau mbalimbali watakaomsadia kuwawezesha
wanawake wa mkoa wake kujikwamua kiuchumi huku akiwasisitizia kuchapa
kazi bila kuchoka wala kubweteka kwa vile wanapata msaada kutoka kwake.
Kwa upande wake, Mbunge wa
Iringa, Tweve aliyemsindikiza Shonza kuzungumza na wanawake hao,
aliwataka wanawake wa Songwe kujivunia mbunge wao (Shonza) kwani ni
mchapa kazi na ni mtu mwenye mtandao npana ambao utawawezesha
kujikwamua kiuchumi.
“kwanza ninawashukuru sana
wanawake wa Momba, na Songwe kwa ujumla kumuamini motto wenu huyu
Shonza, ni muda mfupi nimefahamiana naye. Na hii ni kutokana na uchapa
kazi wake, ninaombe mtumieni vyema bila kusahau na nyinyi kufanya kazi
bila kuchoka.” Alisema Tweve.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya
Momba, Isavera Mwanisenga alisema CCM katika uchaguzi uliopita
walipoteza majimbo yote mawili ya Momba na Tunduma hivyo lakini bado
hawajafa moyo kwani bado wanaye mbunge Shonza anawapigania huku
wakiendelea kujipanga kurudisha majimbo hayo kwenye uchaguzi mkuu wa
mwaka 2020.
0 maoni:
Chapisha Maoni