Apr 29, 2016
KaimuKatibu Mkuu UVCCM |
Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
Umoja
wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Waziri mstaafu
Frederick Sumaye, hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe
na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali
na masuala ya utawala.
Sumaye
ametakiwa amuache Rais Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu
alipewa dhamana ya kuwa Waziri Mkuu lakini hakufikia hata thekuthi ya
utendaji unaofanyika sasa.
Hayo
yamesemwa jana na Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM wa kata mbili za Kwandele na
Mbichi jimbo Rombo mkoani Kilimanjaro.
Shaka
alisema anachokifajya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu
kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka
nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani
wananchi wameyasahau.
Alisema
kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na
usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita
Sumaye.
"Amekuwa
waziri mkuu kwa miaka kumi kuliko waziri mkuu yeyote na kwa bahari
mbaya sana ndiye waziri mkuu zero kuliko mwingine yeyote tokea tupate
uhuru mwaka 1961 "alisema shaka.
Aidha
Kaimu huyo katibu mkuu alimuonya sumaye akimtaka aache kumfuatafuata Dk
Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazichukua
dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.
Alisema
wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi
iuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima alisema kina
sumaye na wenzake wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi
Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.
"Sumaye
aacha kufuatafuata Rais na kujifanya unajua wakati mambo yalikushinda
wakati ukiwa PM, kama huna maneno ya kusema rudi Hanang ukalime maharage
na karanga "alisema
Pia
shaka aliwataka wananchi wa jinbo la Rombo kujitatayarisha ili kumpiga
chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini
kwasabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
"Siku
zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, selasimi hajui
anavhokufanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo
lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisitiza shaka
Akizungumza
katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib
Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya
kushiriki na kuchagua vyama na wagonbea wa nafasi mbali mbali kwa
ukabila, ujimbo au nasaba.
Raibu
alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya
Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi
ya asili au ujamaa.
"Tunachotaka
kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa
Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, haiutuacha tukiwa tumegawahyika
, tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema
acheni kwasabahu hilo ni baa au janga katika jamii "alisema Raib.
Jumla
ya wananchi wapya 103 wa ccm na jumiya zake walijiunga na chama cha
mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya
timu za kata za makiidi na mahare wilaya Rombo.
0 maoni:
Chapisha Maoni