Naibu Katibu Mkuu wa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba (kushoto), Katibu wa Baraza
la Wafanyakazi la Wizara hiyo, Amani Mashaka (katikati), anayefuata ni
Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone wakiwaongoza wajumbe wa
Baraza hilo kuimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya Naibu Katibu Mkuu
kufungua kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga
jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba akizungumza na wajumbe wa
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku
moja wa baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza,
Ukonga, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Balozi Simba aliwataka
watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo
wizara hiyo.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Jeshi la Polisi,
Arcado Nchinga akichangia mada katika kikao cha Baraza hilo
kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar
es Salaam. . Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba (hayupo pichani)
wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe hao katika Mkutano wa Baraza
hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini
Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni