Serikali kupitia wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi
imetoa agizo kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini
kuhakikisha wanafanya ukarabati wavyumba
vya maabala katika shule ya sekondari Tosamaganga kutokana na uchakavu uliopo.
Maabala hayo yamedumu kwa muda mrefu bila kufanyiwa marekebisho na kuakaratiwa hali inayopelekea mabomba ya maji yaliyopo ndani ya vyumba hivyo
kutofanya kazi na kusababisha ugumu wa wananfunzi kujifunza kwa
vitendo .
Agizo hilo limetolewa na waziri wa Elimu na Mafunzo ya
ufundi Dkt Joyce Ndalichako wakati wa ziara yake al;iyoifanya mkoani hapa
juzi na kutembelea shule hiyo kongwe
iliyodumu kwa muda wa miaka 89 toka
ilipoanza mwa 1926 .
Ndalichako alimtaka mgurugenzi na Halmashauri ya Iringa kwa
ujumla wasimamie na wahakikishe
wanaboresha vifaa vyote vya maabala vilivyochakaa
ili wanafunzi waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu sayansi.
.”””””””””””””Tosamaganga
ni shule ambayo tunatakiwa tujivunie watanzania
na inahistoria ndani tan chi na Taifa kwa ujumla.Viongozi wengi
waliowahai kushika nyadhifa mbalimbali nchininn wamesoma katika shule hii,hivyo
hatuna budi kuienzi na kuitunza ili ionekana kuwa ni shule bora hapa nchini lazima iwe na vifaa vya kujifunzia….alisema
Aidha Dkt Ndalichako alizungumza na
walimu wanaofundisha katika shule hiyo na kutoa maagizo kwa kusema kuwa walimu ni wito,hivyo hawana budi kutumia muda
wao mwingi kufundisha kwa bidii ili kiwango cha ufauru kiweze kuongezeka.
Pia alohoji kuhusiana na kushuka kwa
kiwango cha ufahuru kwa wananfunzi katika shule hiyo hivi sasa ukilinganisha na
hapo awali,ambapo shule hiyo pamoja na ukongwe lakini imeshindwa kuingia kwenye
kumi bora katika matokeo ya mitihanai ya kidato cha nne na sita.
“””’’’’’’’’’’’’’Hii hali haivumiliki
kabisa walimu fanyeni kazi mliyoajiliwa na serikali ili Tosamaganga iendelee kutoa viongozi bora na siyo bora
viongozi kutokana na historia yake’’’’’alisema
Alisema wakati serikali inaendelea
kushughulikia madai yao yasiyo ya kimshahara aliwataka kuwa na moyo wa uzalendo
kufundisha bila kuchoka ili kiwango cha ufahuru kiweze kuongezeka.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo
Dismas Mgimwa alimshukuru waziri wa Elimu kwa kuitembelea shule hiyo na kubaini
changamoto zinazoikabili shule na kuahidi kuzishughulikia kwa kuzitatua.
Mgimwa alisema swala la uakarabati wa
vyumba vya maabala ni kilio cha muda mrefu lakinin imeshangwazwa kuonekana
halifanyiwi kazi hali inayopelekea wanafunzi kushindwa kutumia ipasavyo vyumba
hivyo.
Alisema Pamoja na uchakavu wa vifaa na
vyumba vya maabala lakini shule ya Tosamaganga inakabiliwa na uhaba wa walimu
wa sayansina kuseama kuwa ni wachache
ukilinganisha na uhitaji wa wanafunzi,hivyo serikali inatakiwa kuangalia kwa
jicho pevu ili kutatua changamoto hiyo na kuleta uwiano sawa na wanafunzi.
Walimu nao walitoa kilio na malalmiko yao kwa waziri
Ndalichako, ambapo mwalimu Koleta Mfugale
aliiomba serikali iangalia kwa jicho pevu swala la uhaba wa nyumba za
walimu na kusema kuwa kutokanan na changamoto hiyo, wengi wao wanakaa nje ya
shule zaidi ya km kadha hivyo kushindwa
kuleta ufanisi katika kazi.
Mfugale aliitaka serikalai kutoa
tamkoa rasmi la kitaifa kukataza matumizi ya simu kwa wanafunzi hasa katika
shule za sekondari za kutwa na bweni kutokana na wanafunzi waliowengi kumiliki
simu na kupoteza muda mwingi katika
matumizi ya simu za kuliko kujifunza hali inayochangia kushuka kwa kiwango cha ufahurukatika
shule hiyo.
.
0 maoni:
Chapisha Maoni