Na: Immaculate Makilika – MAELEZO.
Tanzania na Oman zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania Chambers of Commerce na Oman Chambers of
Commerce ili kuanzisha Kampuni ya Oman Tanzania Investment (OTIC) kwa
lengo la kutafuta fursa za uwekezaji zili zoko Tanzania na Oman.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa Bibi. Mindi Kasiga amesema kuwa mkataba huo ni
matokeo ya ziara ya siku tatu ya Waziri Viwanda na biashara wa Oman , Dkt. Ally Mohamed Al Sunaidy, pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara 108 na maafisa wa Serikali ya Oman iliyofanyika nchini mwezi Aprili mwaka huu.
Amesema lengo la ziara hiyo
lilikua kuwawezesha wafanyabishara wa Oman na Tanzania kushiriki
kongamamo la biashara la uwekezaji lililowawezesha wafanya bishara hao
kubaini fursa za uwekezaji zilizoko nchini Tanzania na Oman.
Amesema tayari Serikali
ya Oman imeonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha Sukari cha Kagera
kilichopo mjini Morogoro ambacho kitazalisha tani laki nne za sukari
itakayouzwa hapa nchini huku Tanzania ikitarajia kuzalisha spiriti na
hamira itakayouzwa nchini Oman pamoja na nchi za Mashariki ya kati.
‘’ Wafanyabishara wetu na
wale wa Oman kupitia makubaliano haya watanufaika na fursa za uwekezaji
kwa kupata mikopo mbalimbali na tayari mtaji wa Dola za Marekani milioni 25 zitatumika kwa wawekezaji hao’’ Amesema Bibi. Kasiga.
Aidha,amesema
Wafanyabiashara kutoka Oman tayari wameonesha nia ya kuwekeza katika
sekta mbalimbali ikiwemo madini, viwanda na biashara, kilimo, utalii
pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa katika miji ya Dar es Salaam na
Zanzibar.
Ameongeza kuwa uwekezaji
utaongeza ajira akitoa mfano wa kiwanda cha Sukari cha Kagera
kitakachozalisha ajira 500 pamoja na kuongeza wigo wa soko.
Katika hatua amesema kuwa
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa itawapeleka watumishi 105 wa ngazi mbalimbali katika Balozi 35
zilizo katika nchi mbalimbali duniani na kuwarudisha nyumbani
watumishi 79.
Bibi Mindi, ametaja sababu
za kurudishwa kwa watumishi hao kuwa ni pamoja kuisha kwa muda wao wa
kuhudumu nje ya nchi ambao ni miaka minne(tour on duty) pamoja, kustaafu
na sababu mbalimbali.
Amezitaja Kada za watumishi wanaorudishwa nchini kuwa ni mabalozi, wahasibu, makatibu muhktasi na maofisa wa ngazi mbalimbali.
Hata hivyo, hadi kufikia
sasa tayari mabalozi watatu wamerudishwa nchini ambao ni Balozi Peter
Kalaghe aliyekuwa Uingereza, Balozi James Msekela aliyekuwa Italia na
Balozi Batilda Burian aliyekuwa Japan kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa
Januari 25, 2016 kuitaka wizara hiyo kuwarudisha nchini mabalozi
waliomaliza muda wao wa kuhudumu ili wapangiwe kazi nyingine.
0 maoni:
Chapisha Maoni