Ijumaa, 22 Aprili 2016

MWIGULU NCHEMBA AJIKITA KUWEKA MIKAKATI MPYA YA KUINUA KILIMO NCHII,UFUGAJI NA UVUVI


Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mlimba Bi.suzan Kiwanga(CHADEMA) mapema hii leo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mgeta-Mlimba.Moja ya mashine za Umwagiliaji kwenye mashamba ya Mpunga ya KPL(Kilombero Plantation Limited) ikiwa tayari kwa kuanza kazi ya kumwagilia maji kwenye shamba hili la mpunga.Mh.Mwigulu akiangalia sehemu ya mpunga uliohalibiwa kwa kile kinachodhaniwa ni sumu iliyotokana na Umwagiliaji wa sumu aina ya Glyphosate iliyokuwa inatumiwa na wamiliki wa KPL kuchoma nyasi kwenye mashamba yao,
Katika kikao cha pamoja cha wananchi,Uongozi wa serikali na uongozi wa KPL(Kilombero Plantation Limited),Mwigulu Nchemba amepokea hatua za awali za wataalamu na watafiti wa serikali waliobobea kubaini chanzo cha mimea kuharibika kwa kiasi kikubwa hivi,Wataalam hao wamemhakikishia Mh.Mwigulu Nchemba kuwa watatoa ripoti yao kamili ndani ya muda wa siku 21 ili kubaini aliyesababisha mimea ya mpunga kuungua.
Mwigulu Nchemba amewahakikishia wananchi kuwa serikali ya Rais.Magufuli imejipanga kutetea haki za wananchi na itamuwajibisha yeyote anayehujumu kilimo na ustawi wa Taifa letu
Vilevile Mh.Mwigulu Nchemba alifanikiwa kupitia shamba la Ruaha ambalo lipo chini ya muwekezaji kotaka nchini Marekani,hapa akipata maelekezo namna kilimo kinavyotakiwa kuendana na wakati.Utofauti wa Kilimo cha kisasa cha kuzingatia mbolea,Mbegu na wakati na kilimo cha kiholela ambacho hakizingatii mbegu na mbolea.Moja ya trekta la kisasa la muwekezaji wa "Ruaha Farm" ambalo linatumika kupanda mbegu,kuvuna na mwagilia dawa ya mimea.Waziri wa Kilimo akipewa maelezo kuhusu uhudumiaji wa mashamba ya Mahindi kuanzia uaandaji wa shamba,mbegu,mbolea na majira ya kupanda mahindi.
Wakati wa ziara hiyo,Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya kilimo ameendelea kusisitiza kuwa kuna haja kama Taifa kuachana na kilimo cha jembe la mkono,lakini matumizi ya mbegu bora na mbolea bora ni muhimu yazingatiwe.
Wizara inajipanga kuandaa mfumo mzuri wa kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa kupata pembejeo kwa wakati na upatikanaji wake uwe rahisi.
Lakini,Mwigulu Nchemba pia amewasihi sana wawekezaji kwenye mashamba n.kuheshimu taratibu za uwekezaji,ili kuondoa mahusiano mabaya kati ya muwekezaji na wananchi.

0 maoni:

Chapisha Maoni