Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa
viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya
shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika
kuwalipia michango ya mwezi.
Semina
hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar
es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa
vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege.
Katika
hotuba yake, Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango
wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi
wapatwapo na majanga wakiwa kazini.
Mfuko
wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya
Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia
kwa wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008.
Akiwakaribisha
wana semina kwenye semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha
Msomba alisema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi
kwa wafanyakazi na kwa kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau
wakuu wa Mfuko huo, semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini
pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila
mwezi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza
wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi
wa vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko,
barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2016. Lengo la
semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao juu ya shughuli za
Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo patatokea madhara
awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege,
(Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J.
Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya
jamii, (SSRA).
Akitoa
mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa
fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
Naye
Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa
Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa
wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu
wa kutoa michango kwa wakati.
Mshiriki akisoma kijitabu
chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya maswali ya mara kwa mara
ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF.
Bi. Pendo Berege, akifungua semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka,
akitoa hotuba ya kufunga semina hiyoMkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba.
Bi. Irene Isaka
Mzee Mchafu Chakoma, mwakilishi wa viongozi wa wafanyakazi akitoa neno la shukrani.
Bw. Chakoma (kushoto), akibadilihana mawazo na Bi. Pendo Berege
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akitoa mada “Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF)
Bi. Pendo Z.Berege,
(kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Ukauzi wa ndani cha Mamlaka ya Udhibiti
na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).Peter J. Mbelwa,
wakiteta jambo.
Majadiliano yakiendelea
Mmoja wa washiriki wa semina akizungumza kwenye kipindi cha majadiliano cha semina hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakichukua taarifa muhimu
Mshiriki akifuatilia kwa makini
0 maoni:
Chapisha Maoni