Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki akikabidhi madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66
kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya yaliotolewa na
Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George
Lugata.
Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Meck Sadiki(Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya(katikati) Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.………………………………………………………………………….
Kampuni
ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya
shilingi milioni 66 kwa shule nane za msingi katika manispaa ya Mwanga,
mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia
serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi
nchini.
Akizungumza
leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi
Reli Juu katika manispaa ya Mwanga, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya
Kaskazini George Lugata amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji
wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta
maendeleo nchini.
“Mchango
huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika
kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini
kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika
kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali
wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Lugata.
Lugata
amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika
shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na
kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu
mbalimbali nchini siku za zijazo.
Makabidhiano
yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mheshimiwa Meck Sadiki
ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa
watoto katika Mkoa wa Kilimanjaro na kutoa wito kwa wadau wengine
kuunga mkono zoezi hilo.
“Tunapenda kutoa
shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu
kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la
ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa
Kilimanjaro. Ni dhahiri
kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Sadiki
Madawati hayo yametolewa kwa shule za msingi nane kama ifuatavo, Mramba,Kawawa, Mwanga, Naweru,Kiboriloni, Lawate na Reli Juu.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni