Mkurugenzi
Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu
(UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa
zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa
PSSN wa TASAF.
(Picha na Modewjiblog)
………………………………………………………………………………………………………
Washirika
wa maendeleo nchini wametembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito
vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya
masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo washirika hao wamekuwa
wakitoa fedha ili kusaidia miradi hiyo.
Washirika
hao wa maendeleo kutoka UN Tanzania, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya
Serikali ya Uingereza (DFID), Irish Aid, USAID na Shirika la Kimataifa
la Misaada la Sweden (SIDA) ambao wamekuwa wakishirikiana na TASAF
katika Mpango wa Kusaidia Kaya Masikini (PSSN).
Wakitoa
taarifa mbele ya washirika wa maendeleo, wanavikundi kutoka Kijiji cha
Vikuge wamesema kuwa kupitia mpango huo wameweza kuboresha maisha yao
tofauti na jinsi ilivyokuwa awali.
Walisema
kuwa maisha yao ya awali yalikuwa magumu lakini kutokana na msaada
walioupata kutoka TASAF wameweza kuanzisha vikundi ambavyo vinawasaidia
kuboresha maisha kwa kufanya biashara za mazao, nguo na chakula.
“Kuna
mafanikio tumeyapata darasani mahudhurio yameongezeka, klini wamama
wanakwenda na hata utapiamlo haupo tena kwa watoto kwa sababu ya TASAF
kutusaidia,” alisema mwakilishi wa wanavikundi kutoka Vikuge.
Mratibu
TASAF Kibaha, Goodson Hare, akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe wa
washirika wa maendeleo nchini waliotembelea vijiji viwili Vikuge na
Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya
kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo
zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumzia
ziara hiyo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa MATAIFA NCHINI, Alvaro Rodriguez
alisema wamefanya ziara hiyo ili kuona ni hatua gani imefikiwa na
wanufaikaji na kuona ni changamoto gani bado zinawakabili.
“Tunaangalia
changamoto zilizopo ili kuona ni jisni gani tunaweza kuwasaidia kama
Mpango wa Kusaidia Kaya masikini ulivyo nab ado kuna wahitaji zaidi
licha ya kuwa tumeshasaidia kaya Milioni1.1 kwa nchi nzima,
“Mpango
huu ni mzuri na kawa wasaidiwa wakiwa kama wajasiliamali na kutengeneza
kipato inaweza kusaidia Tanzania kuondokana na umasikini kuelekea
katika uchumi wa kati kama jinsi ilivyojiwekea malengo,” alisema
Rodriguez.
Kiongozi
wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini, Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),
Alvaro Rodriguez akizungumzia madhumuni ya ziara yao kwa wanakijiji.
Mkurugenzi wa Programu Jamii wa TASAF, Amadeus Kamagenge akizungumza jambo wakati wa utambulisho wa ujumbe huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni