………………………………………..
Mkuu
wa mkoa wa MWANZA John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi
Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa,kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata
komputa iliyo ibwa usiku wa kuamkia April 22,2016 kwenye chumba kinacho
tumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya
Halmashauri (EPICOR)
Mongella
ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha
kilicho fanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali
zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba
cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya
halmashauri.
“OCD
kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka
taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana,amesema Mongella
na kuongeza ,sisi tunajua Nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na
usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi
ilipo komputa hiyo.
Akizungumza
kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri,kaimu mhazini wa halmashauri
hiyo Baraka Munuo,alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo
kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe akimuelezea upotevu
huo.
Katika
hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya ukerewe,, kupitia mafaili na kubaini watumishi
waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa
mkoa amedai linachangiawatumishi kufanyakazi kwa mazoea,”Mkurugenzi
nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika
kituo hiki kwa muda mrefu, haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishini na
moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana, alisema
Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna
mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.
Awali
akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph
Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni
shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema
wilaya imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa
kimepiga kambi katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.
Mkuu
wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya
yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu,
Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba
huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za
Buchosa na Sengerema yenyewe.
0 maoni:
Chapisha Maoni