Jumapili, 24 Aprili 2016

MASHINDANO YA RIADHA YA VIJANA CHINI YA MIAKA 19 YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI (EAAR)

ria
MASHINDANO ya riadha ya Vijana chini ya Miaka 19 ya Afrika Mashariki na Kati (EAAR), ambayo yatafanyika Aprili 29 na 30 jijini Dar es Salaam, yanatarajiwa kuoneshwa ‘live’ Azam TV.
Mashindano hayo yatafanyika Uwanja wa Taifa, huku yakishirikisha nchi tisa huku Tanzania Bara wakiwa wenyeji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla, alisema kwamba wapenzi wa riadha ambao wapo mbali na Dar es Dar es Salaam watafaidika kuona mashindano hayo kupitia televisheni hiyo.
Zavalla, aliupongeza uongozi wa Azam TV kwa kitendo chao cha kiunamichezo ambacho kitachangia kuhamasisha kuendeleza mchezo hapa nchini sambamba na kuitangazaTanzania kimataifa.
Alisema mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha nchi za Tanzania Bara, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda,Rwanda, Sudan, Ethiopia, Eritrea na Zanzibar.
Alisema mwisho wa nchi kuthibitisha ilikuwa juzi usiku na timu zote tayari zimethibitisha isipokuwa Sudan Kusini.
“Kwa sababu muda umekwisha na hatujapata uthibitisho kutoka Sudan Kusini wala taarifa zozote basi itakuwa imejitoa kwenye mashindano hayo hivyo zimebaki nchi kumi,” alisema.
Alisema kwamba wao kama waandaaji, tayari wamekamilisha kila kitu na timu ya Tanzania Bara iko kambini ikiendelea kujifua.
“Timu imeingia kambini wiki iliyopita katika hosteli za Filbert Bayi huko Kibaha, Pwani, ikiwa na jumla ya wachezaji 27 ambao wana afya nzuri na wapo tayari kwa mashindano hayo,” alisema.

0 maoni:

Chapisha Maoni