Alhamisi, 28 Aprili 2016

Shule inayodidimia baharini Ghana


Nyumba nyingi katika pwani ya jimbo la Volta huko Ghana zimeharibiwa na mawimbi katika kipindi cha wiki moja iliopita.
Shule hii ilikuwa mbali na ufukwe wa bahari miaka michache iliopita lakini sasa imedidimia ardhini.

Kulikuwa na wanafunzi 54 katika shule hii lakini sasa hawana madarasa.Hatma ya elimu yao haijulikani.
M'momonyoko unaosababishwa na bahari umeharibu vijiji katika ufukwe wa bahari ya Afrika Magharibi ,na kutishia jamii zote.
Watu katika jamii wamesema kuwa iwapo hakuna kitakachofanyika miji yao itaangamizwa.

0 maoni:

Chapisha Maoni