Ligi
hiyo ya mabingwa wa mikoa itachezwa katika vituo vine nchini, ambapo
mshindi wa kila kundi atapanda moja kwa moja ligi daraja la pili (SDL)
na mshindi wa pili mwenye matokeo mazuri kutoka kundi A, B na C.
Kundi
A kituo cha (Njombe) kutakua na mabingwa wa mikoa ya Ruvuma, Iringa,
Mbeya, Rukwa, Katavi, Dar es salaam 3, Morogoro, Kundi B kituo cha
(Morogoro) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi, Dar es
salaam 1, Dar es salaam 2, Tanga, na Singida.
Kundi
C kituo cha (Singida) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Dodoma, Arusha,
Kilimanjaro, Tabora, Kagera, Manyara, na Njombe, huku kundi D kituo cha
(Kagera) kikiwa mabingwa wa mikao ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu,
Mara na Kigoma.
SDL LIGI NDOGO KUANZA MEI 11
Timu
zilishoshika nafasi ya pili katika msimamo wa SDL kwa kila kundi,
Abajalo FC (Dar es salaam), Pamba FC (Mwanza), Mvuvumwa (Kigoma), Mighty
Elephant (Songea) zitacheza ligi hiyo kusaka timu mbili zitakazoungana
na timu nne za juu kupanda ligi daraja la kwanza (FDL) msimu ujao.
Klabu
nne za Allicane Schools (Mwanza), Mshikamano FC (Dar es salaam), Mbeya
Warriors (Mbeya) na Singida United (Singida) zilizoongoza msimamo wa
makundi ya SDL zitaungana na timu mbili kupanda ligi daraja la kwanza
msimu ujao.
0 maoni:
Chapisha Maoni