Timu
ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania Bunge
Sports Club inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo mkali na wa aina
yake ambao ni wa kwanza na timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Mapema
leo Aprili 25.2016 timu hiyo ilishuka katika dimba hilo la Amani na
kupasha misuli maalum kwa hiyo mchezo huo wa hiyo kesho ambapo kwa
mujibu wa viongozi wa timu hiyo ya Bunge wametamba kuibuka na ushindi wa
kishindo.
Kocha
wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh.
Venance Mwamotto ametamba kwa timu yake kuibuka na ushindi mnono katika
mchezo huo kwani wana mazoezi ya kutosha na pia wamejiandaa kuonyesha
uwezo.
“Tunawaomba
wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya
kutosha kuhakikisha tunashinda. Mchezo huu ni maalum kwa ajiri ya
kuimalisha Muungano wetu tukufu hivyo tutaendelea kuuenzi na kuukumbatia
na sote kwa pamoja tuzidishe Amani” alieleza Mh. Mwamotto.
Kwa
upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani ‘Maji
Marefu’ ambaye ni miongoni mwa viongozi wa msafara wa timu hiyo ya
Bunge ametamba timu yake kuibuk na ushindi mnono kwani wamejiandaa
kisaikolojia na mazoezi ya kimichezo.
Naye
Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla viongozi
wa timu hiyo ya Bunge amebainisha kuwa, mchezo huo unatarajiwa
kuchezwa majira ya Saa 12 Jioni kesho Aprili 26.2016 katika uwanja huo
wa Amani.
“Mechi
kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza
la Wawakilishi la Zanzibar. Utachezwa kesho ni siku ya Kuadhimisha
Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar. Tunawaomba watu kujitokeza kwa wingi kuuona mchezo huu ambao
utakuwa wa aina yake kwa timu zote mbili.” Alieleza DK. Kigwangalla.
Timu
hiyo ya Bunge yenye wachezaji Zaidi ya 19 imejiandaa vya kutosha katika
kuakikisha inapata ushindi mnono na ipo Visiwani hapa kwa maandalizi ya
mchezo huo tokea jana na leo imeweza kufanya mazoezi ya awali asubuhi
na mengine wakitarajia kufanya hapo jioni.
Timu ya Bunge ikifanya mazoezi yake mapema leo Aprili 25 kuajiandaa na mchezo huo utakaochezwa keshi Jioni uwanja wa Amani.
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’ akisimamia mazoeszi hayo kwa muda wakati wsa asubuhi ya leo
mazoezi hayo yakiendelea..
Mazoezi yakiendelea
Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto (kati) akitoa maelezo ya mazoezi hayo
Benchi la ufundi likiwa tayari katika mazoezi hayo
Mbunge William Ngeleja akijaribu kutaka kuchukua mpira kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mazoezi moto moto yakiendelea..
Mazoezi
makali ya timu ya Wabunge yakiendelea katika uwanja wa Amaan, Unguja
leo Aaprili 25.2016. Timu hiyo kesho Aprili 26 inatarajia kucheza mchezo
wao dhidi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. (Picha zote na Andrew
Chale,Modewjiblog, Zanzibar).
0 maoni:
Chapisha Maoni