Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar kushoto akikabithiwa
nyaraka na Katibu Mkuu Mstaafu Ali Mwinyikai katika makabidhiano
yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na
Michezo Mnazi Mmoja Zanzibar .
…………………………………………………………………………………………………
Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Omar Hassan
Omar amesema azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuwapatia
wafanyakazi wake huduma bora ili waweza kundeleza kazi zao kwa
ufanisi.
Hayo ameyasema leo huko katika
ukumbi wa Wizara Mnazi mmoja baada ya kukabidhiwa Ofisi na Katibu
Mkuu aliemaliza muda wake Ali Mwinyikai .
Amesema utendaji kazi wa
Serikali ni wapamoja na sio mtu mmoja mmoja hivyo aliwaomba viongozi
na wafanyakazi wa wizara kumpa mashirikiano makubwa katika utendaji wa
majukumu yake.
Katibu Mkuu alisema Wizara ipo
katika hali nzuri kiutendaji hivi sasa na ameahidi kufanyakazi kwa
juhudi kuweza kupata ufanisi zaidi na kuleta maendeleo.
Amesema yuko tayari kupokea
ushauri na kukosolewa na wafanyakazi wenzake na amewahakikishia
kwamba watashirikiana ili waweze kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali
katika Wizara hiyo.
“Sisi viongozi peke yetu hatuwezi
kufika mbali katika kuleta maendeleo bila ya mashirikiano ya pamoja
hivyo mashirikiano ya pamoja ndio mafanikio yetu sote,” alisema Katibu
Mkuu.
Ameahidi kusimamia na kudhibiti
matumizi ya fedha ya Wizara ili kuongeza mapato na kuimarisha Idara ,
Taasisi na kuboresha maslahi hasa ya taaluma kwa wafanyakazi .
Amesema Wizara ni kubwa na
imebeba taasisi muhimu katika maendeleo ya ikiwemo habari, utalii ambao
ni tegemeo kubwa kwa taaifa kwa sasa, utamaduni na michezo pia ni
kielelezo muhimu cha Taifa.
Nae Katibu Mkuu mstaafu Ali
Mwinyikai amemuhakikishia Katibu Mkuu mpya kuwa yupo tayari kumpa
mashirikiano ya kila hali ili kazi za Wizara ziende kwa kasi zaidi.
Pia aliwashukuru viongozi wenzake
wa Wizara kwa kumpa mashirikiano mazuri katika utendaji wa kazi zake
na aliwaomba kumpa mashirikiyano katibu wao Mkuu wa sasa ili aweze
kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu
Mkuu mstaafu Issa Mlinngoti akimkabidhi Naibu katibu mkuu mpya Amina
Ameir Issa Ofisi amesifu mashirikiano aliyoyapata kutoka kwa wafanyakazi
wenzake na kuwaomba waendelee kumpa mashirikiano Naibu mpya ili kazi
zake ziende vizuri.
0 maoni:
Chapisha Maoni