Rais
wa VICOBA Devotha Likokola amewaasa wafanyakazi waliopo kwenye ajira
hususani wanawake kujiunga na vikundi vya VICOBA ili waweze kujikwamua
kimaisha na kuboresha maisha ya familia zao.
Bi.Likokola
alitoa wito huu jana wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake
wanaofanya kazi katika kampuni ya DarBrew inayotengeneza kinywaji cha
Chibuku iliyofanyika katika kiwanda cha Dar es Salaam.
Alisema
kwa kujiunga na VICOBA wanawake hao watakuwa na uwezo wa kupata mikopo
yenye masharti nafuu na kupata mafunzo ya fursa mbalimbali za kibiashara
zilizopo na kuwakutanisha na wanawake wenzao ili waweze kubadilishana
uzoefu wa maisha.
“Kuna
dhana kwamba VICOBA ni kwa ajili ya akina mama wasio na ajira na
wanawake wengi walioajiriwa kutotaka kujiunga na vikundi hivi kwa ajili
ya kuwakwamua kiuchumi matokeo yake waajiriwa wengi wanaachwa nyuma
kiuchumi kutokana na kutegemea mshahara wa mwisho wa mwezi tu”.Alisema
Likokola.
Rais
wa Vicoba endelevu Tanzania, Devotha Likokola, akitoa mafunzo ya elimu
ya vicoba kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha Chibuku (Darbrew Ltd) cha
Ubungo jijini Dar es Salaam.
Aliwaasa
wanawake kuchangamkia fursa hii ambayo pia imeanza kuchangamkiwa na
wanaume na kuwataka waajiri kuwezesha wafanyakazi wao kupata mafunzo ya
ujasiriamali ili yawaandae kujiajiri baada ya muda wao wa ajira
kumalizika na hata wakiwa makazini bado kuna shughuli mbalimbali za
ujasiriamali wanaweza kuzifanya kwa ajili ya kuinua vipato vyao.
Katika
mafunzo hayo wanawake wafanyakazi wa DARBREW walipatiwa mwongozo wa
kujiunga na vikundi vya VICOBA ambapo pia walipatiwa elimu ya
ujasiriamali,jinsi ya kuibua miradi na kuiendesha pia walipatiwa ushauri
wa jinsi ya kutumia fedha kwa malengo ya kufanikiwa na umuhimu wa
kujiwekea akiba.
VICOBA
ambayo ilianzishwa ikiwa na mtizamo wa kusaidia vikundi vya wanawake wa
vijijini kiuchumi imezidi kupanua huduma kwa wanawake wengi nchini
ambapo hivi sasa inao mtandao wa vikundi zaidi ya 10,000 nchi nzima
vyenye wanachama zaidi ya 500,000 na mtaji unaofikia zaidi ya shilingi
bilioni 75.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Chibuku (Darbrew Ltd) wakimsikiliza Rais wa Vicoba endelevu Tanzania, Devotha Likokola.
Mratibu wa Vicoba mkoa wa Dar es Salaam, Amina Mkuwa (kulia) akigawa vipeperushi vya taasisi hiyo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Chibuku (Darbrew Ltd) wakisoma katiba ya Vicoba.
Wafanyakazi
wa Chibuku (Darbrew Ltd) Ubungo jijini Dar es Salaam, wakiwa katika
picha ya pamoja na Rais wa Vicoba endelevu Devotha Likokola mara baada
ya kumalizika kwa mafunzo.
0 maoni:
Chapisha Maoni