Vikundi vya mazoezi vikiwa katika
matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo
yamefanyika kuanzia Mazizini Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia
Maisara Mjini Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (katikati) akiongoza Matembezi ya hiari ya
kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia mazizini
na kumalizikia maisara mjini Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya
Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kushoto yake ni katibu Mkuu Wizara ya
Afya Dkt Juma Malik Akili.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi
vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika
maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika Mjini Unguja.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi
vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika
maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika Mjini Unguja.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo (wa mwanzo ) akishiriki katika mchezo wa kuvuta kamba kwenye
maadhimisho hayo ambapo timu ya Baraza la Wawakilishi ilipambana na
Wizara ya Afya ambapo Afya ilipata ushindi.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria
Duniani ambayo yamefanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Maadhimisho ya siku ya
Malaria Duniani ambayo yamefanyika Maisara Mjini Unguja.kulia yake ni
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na Kushoto yake ni Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
……………………………………………………………………………………………………
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amewataka wananchi wa wanaosafiri mara kwa mara kwa ajili ya harakati
zao za maisha kuchukua vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili
kujikinga na maradhi ya Malaria.
Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani
katika viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema licha ya
Zanzibar kuwa na kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria,
utafiti unaonyesha watu wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni
wale wenye utaratibu wa kusafiri nje ya Zanzibar.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa
dhati kuimarisha afya za wananchi na itaendelea kuboresha huduma za afya
sehemu zote na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
Hata hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia mafanikio
katika vita dhidi ya Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea
kuwa tishio kwa wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na
wataalamu wa afya.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik Akili alisema
katika kumaliza Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa vyandarua
760,000 vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote za
Zanzibar.
Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.
Katika maadhimisho hayo, wananchi na vikundi vya mazoezi
wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari
yaliyoanza Mazizini, Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya
Maisara, Mjini Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni