-Ashauri vijana wasikimbie kilimo na masomo ya sayansi na ufundi.
Wakati
nchi yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kupiga hatua kiuchumi
na kusababisha wananchi wengi kubaki maskini, wapo baadhi ya watanzania
wana maono kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za kuondokana na umaskini
bali tatizo lililopo ni wananchi wengi kutowajibika ipasavyo hususani
katika kufanya kazi wanavyostahili.
Calvin
Martin, Meneja wa kiwanda cha kutengeneza Bia cha Tanzania Breweries
kilichopo jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa watanzania wanaoamini
kuwa nchi yetu inazo fursa nyingi za kuondokana na umaskini, kuboresha
huduma za kijamii na wananchi kuishi maisha mazuri.
Ana
imani kuwa falsafa ya ‘Hapa Kazi tu’iliyoanzishwa na Rais wa awamu ya
tano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli, ikitekelezwa ipasavyo nchi yetu
itapiga hatua kubwa kiuchumi kwa kuwa upo ushahidi wa baadhi ya
mataifa hususani barani Asia ambayo kwa kupitia falsafa kama hii
wameweza kupiga hatua kubwa kiuchumi kwa haraka.
Katika
mahojiano hivi karibuni Calvin alisema kuwa ana imani kuwa mtu yeyote
akifanya kazi kwa bidii na maarifa ni lazima afanikiwe katika jambo
lolote na imani hiyo imemsaidia kufanikiwa katika mambo mengi hadi
kufikia hatua alipo ya kuwa Meneja wa kiwanda cha kutengenezwa vinywaji
chini cha Tanzania Breweries.
“Siku
zote naamini kuwa kufanya kazi kwa bidii na ueledi kunaleta mafanikio
na huwa nasikitika sana kuona baadhi ya watu hususani vijana ambao
wanakaa bila kufanya kazi wakati wana nguvu za kutosha na nguvu kazi
inapotea bure badala ya kushiriki katika uzalishaji kwa manufaa yao na
manufaa ya taifa”. Alisema.
Alisema
kuna umuhimu mkubwa wa kuwajengea watanzania mazingira mazuri ya
kufanya kazi ziwe kwa kuajiriwa ama kujiajiri wenyewe na kuongeza kuwa
ajira nyingi ziko katika sekta ya kilimo, ufugaji, viwanda na kwenye
ufundi wa aina mbalimbali.
Calvin
alisema kuwa amepata elimu ya juu katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
ambako alisomea shahada ya kwanza ya Sayansi na alikuwa miongoni mwa
wahitimu waliofanya vizuri katika mwaka 1993
Baada
ya kumaliza masomo ya Shahada ya kwanza Chuo Kikuu, alijiunga na
masomo ya Shahada ya uzamili chuoni hapo akijikita zaidi katika Sayansi
ya viwanda na utawala ambako alihitimu mwaka 1997.
Ajira
yake ya kwanza ilikuwa katika kampuni ya East Africa Breweries ambako
alikuwa kwenye kitengo cha uzalishaji na kwa muda mfupi aliweza kuielewa
fani ya uzalishaji bia kwa vitendo na nadharia, kuhitimu Stashahada ya
utengenezaji bia (Diploma in Brewing) ya Uingereza na baada ya kufanya
kazi na kampuni hiyo kwa miaka mitatu na nusu aliamua kujiunga na
kampuni anayofanyia kazi kwa sasa hivi ya TBL Group.
Calvin akimtembeza Afisa Mwandamizi wa SABMiller, Olga Luskotova alipofanya ziara nchini hivi karibuni.
Akiwa
na kampuni hii ameweza kushika nyadhifa mbalimbali hadi kufikia nafasi
aliyonayo hivi saa ya kusimamia kiwanda kikubwa cha TBL Cha Dar es
salaam. Moja ya kazi kubwa anazojivunia nazo ndani ya kampuni hiyo ni
kusimamia ujenzi na uanzishwaji wa kiwanda cha Mbeya.
“Kazi
ya kuanzisha kiwanda hiki ilikuwa moja ya changamoto ya kikazi kwangu
lakini kutokana na ujuzi na uzoefu kwa kushirikiana na wenzangu
tulifanikiwa na najivunia kuona kiwanda hiki ni moja ya viwanda vya
kampuni vinavyofanya vizuri kikiwa chini ya uongozi na wafanyakazi
watanzania.
Mbali
na kupata elimu za vyuoni akiwa mwajiriwa wa TBL tayari Calvin
amehudhuria kozi mbalimbali ndani ya kampuni ndani na nje ya nchi
ambazo zimezidi kumpatia maarifa ya kitaalamu, kiufundi, utawala,
uendeshaji na usimamiaji wa viwanda kwa ufanisi.
“TBL
kuna mafunzo ya aina nyingi na kuna mitambo ya kisasa na mara nyingi
tumekuwa tukipata mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo ya mifumo ya
uendeshaji viwanda kwa ufanisi mfano ‘SABMiller Manufacturing Way’
ambayo tunaitumia na imeonyesha mafanikio makubwa.
Pia
alisema kuna mafunzo ya utawala na mifumo mbalimbali inayowawezesha
Mameneja wa viwanda na wakuu wa vitengo kuendesha shughuli zao vizuri
wakiwa wanajua jinsi ya kutoa vipaumbele kwenye mambo mbalimbali na
mpangilio mzuri wa ratiba za kazi.
Calvin
aliongeza kusema kuwa anaweza kufanya kazi zake vizuri kutokana na
ushirikiano mzuri anaopata kutoka kwa wafanyakazi wenzake “TBL ni tanuru
la kupika wataalamu na imeajiri watu wenye uwezo mkubwa katika fani zao
hivyo nafanya kazi na wataalamu ambao wana upeo mkubwa na wanaoelewa
nini wanachokifanya, wanaojituma bila kuhitaji usimamizi mkubwa.
Kuhusu
changamoto anazokumbana nazo katika kazi yake alisema ni za kawaida na
kutokana na elimu yake na uzoefu wa kazi alionao anaweza kuzitatua kwa
urahisi na maisha kuendela kama kawaida.
Calvin Martin akimwonyesha Waziri wa Viwanda na Biashara,Charles Mwijage alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.
Anasema
anajivunia kufanya kazi na kampuni kubwa kama TBL Group ambayo
imemuwezesha kujifunza mambo mengi ikiwemo kupata mafanikio mbalimbali
katika maisha yake mojawapo ikiwa ni kuihudumia familia yake vizuri.
Alimalizia
kwa kutoa wito kwa vijana wa kitanzania kutokimbia masomo ya hesabu na
sayansi wanapokuwa mashuleni bali wajitahidi kukomaa nayo kwa kuwa
katika dunia hii ya sayansi na teknolojia bila wataalamu katika nyanja
hii itakuwa vigumu kwa taifa kupiga hatua ya maendeleo na muda wote
wajue kuwa mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii.
0 maoni:
Chapisha Maoni