Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari
kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo kwa kufanyakazi chini
ya kiwango pamoja na wasaidiziwake wawili.
…………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es
Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya ujenzi, Mhandisi Japhery
Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa
barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo,
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja maofisa
wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na Daniel
Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi
unaoendelea.
Kuyeko
alisema kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada ya
manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa
ujenzi wa barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo.
Alisema
baada ya kuingia madarakani kwa miezi mitatu walijaribu kutafuta kero
ndani ya manispaa ya Ilala ambapo walibaini idara ya ujenzi ina
malalamiko mengi kutoka kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa sababu ya
kusimamia ujenzi wa barabara chini ya kiwango na hakuna hatua stahiki
zilizochukuliwa na maofisa hao.
Alisema
madiwani hao walimlalamikia Mhandisi Bwigane kuwa amekuwa akikaidi wito
wao wa kujadili ujenzi wa barabara mbovu pindi zinapobainika jambo
ambalo limesababisha manispaa hiyo kuwa na barabara nyingi mbovu.
Jitihada
za gazeti hili za kumtafuta Mhandisi Bwigane ili kuzungumzia
kusimamishwa kwake kazi hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake na
wakati wote kuwa imefungwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni