Na Beatrice Lyimo – MAELEZO
Dar es Salaam
……………………………………………………………………..
Wadau mbalimbali kutoka vyama
vya Siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25,
2015 wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendesha zoezi
hilo kwa Uwazi, Haki, Amani na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni.
Hayo yamesemwa leo na Katibu
Mkuu wa Chama cha NRA Bw. Hassan Kasabya alipokuwa akitoa pongezi kwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kutoa vyeti vya shukrani kwa washiriki hao
katika huo kwa vyama vya siasa na wadau wengine.
Bw. Kasabya amesema kuwa Taifa
ya Uchaguzi (NEC) iliona umuhimu wa vyama hivyo kama wadau wa uchaguzi
na chaguzi zote hapa nchini na kuamua kutoa kutoa vyeti vya shukrani kwa
kufanikisha uchaguzi huo.
“Vyeti hivi ni kielelezo tosha
cha umakini wa Tume yetu na jinsi gani wamejali na kuthamini ushiriki wa
vyama vyetu, kwani pasipo vyama vyetu hivi uchaguzi mkuu hauwezi
kufanyika” ameongeza Katibu Mkuu huyo.
Aidha, kwa upande wake Katibu
Mkuu kutoka Chama cha AFP Rashid Rai ametoa wito kwa Serikali kuzidi
kuiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi hususan uboreshwaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura na kuzidi kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura.
Mbali na hayo, Wadau hao
wameipongeza Tume hiyo kwa mabadiliko makubwa ya kiutendaji
yaliyofanyika katika uchaguzi mkuu uliopita kulinganisha uchaguzi wa
mwaka 2010, 2005, 2000 na 1995.
Wadau walioshiriki kuipongeza
NEC kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ni pamoja na Chama cha
National Alliance and Reconstruction (NRA), Chama cha Alliance for
Tanzania Farmers (AFP), Chama cha United Peoples Democratic Party
(UPDP), Chama cha UMD, Chama cha Demokrasia Makini (MAKINI) na Chama cha
Haki na Ustawi (CHAUSTA).
0 maoni:
Chapisha Maoni