Alhamisi, 28 Aprili 2016

Trump atangaza sera zake za nje


Donald Trump anayewania kuteuliwa na chama chake Republican kuwania Urais nchini Marekani ametangaza sera zake za nje.
Trump ametoa hotuba yake ya kwanza inayohusu sera za mambo ya nje na kugusia maeneo mbalimbali ikiwemi mapambano dhidi ya ugaidi na mpango wa nyuklia wa Iran.

Amezungumzia pia kuhusiana na mahusiano ya nchi hiyo na Israel, Urusi na China.
Katika hotuba yake hiyo pia ameishambulia vikali sera hiyo chini ya utawala wa Rais Barack Obama.

0 maoni:

Chapisha Maoni