Jumatano, 20 Aprili 2016

Wito kwa Wasanii kushiriki tamasha la Sauti za Busara 2017


Sauti za Busara ni tamasha lifanywalo kila mwaka mwezi wa Febrauri Zanzibar, huonesha muziki wa Afrika yote na kwengineko. Tamasha hilo limo kwenye mtandao wa CNN ilitoa orodha ya matasha 7 ya Afrika ambayo yanamvuto wa kipekee kuyaona.
Pia tamasha la Sauti za Busara limo kwenye matasha 25 bora ya kimataifa na mtandao wa kitalii wa Afro Tourism’s umeliingiza tamasha hili katika matasha 8 bora ya muziki. Na mwezi wa Februari 2015, BBC World Service imelitaja tamasha la Sauti za Busara kama ni ‘moja kati ya matukio muhimu na yenye kuheshimika barani Afrika.
Mwisho wa kupokea maombi kwa wasanii wote ni 31 Julai 2016
Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri, malazi, chakula na matumizi madogo madogo. Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri
Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2017. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi wa tisa

Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2017

Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutayapokea kabla tarehe 31 Julai. Maombi yako lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:
  • fomu ya maombi iliyojazwa mtandaoni na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
  • nakala moja au mbili ya kazi zako za hivi karibuni (CD au DVD)
  • picha moja au mbili(Picha zinaweza kutumwa kwa journey@busara.or.tz)
Bonyeza hapa kwa fomu ya maombi.
Tafadhali tuma nakala,picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo chini. Vitu vyote vitakavyotumwa lazima viaandikwe FOR PROMOTIONAL USE ONLY.
IMG_930113064015_1155280531189525_242843889_o

0 maoni:

Chapisha Maoni