Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa Joachim Mshana akisoma matatizo yaliyopo katika kijiji cha
Makatapola Kata ya Migoli tarafa ya Isimani kwa mujibu wa tathmini
zilizofanyika wa wa PRA wakati wa Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Makatapola
jana.
Mrasimu Ramani (Cartographer) wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Geoffrey Mwanga akisoma mapendekezo ya
sheria ndogo za kusimamia mpango shirikishi jamii wa matumizi bora ya
ardhi ya kijiji cha Makatapola Kata ya Migoli tarafa ya Isimani,
zilizotayarishwa na kamati ya matumizi bora ya ardhi ya kijiji cha
Makatapola, na kupishwa jana na halmashauri ya kijiji na mkutano mkuu wa
kijiji. Mpango umefadhiliwa na WWF na halmashauri ya wilaya ya Iringa.
Mkazi mmoja wa kijiji cha Makatapola
Kata ya Migoli tarafa ya Isimani akipiga kengele kwa ajili ya
kukaribisha wananchi katika mkutano mkuu wa kijiji hicho.
Afisa Mipango miji na vijiji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Zahoro Mwalongo akifafanua jambo wakati
wa Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Makatapola jana.
Mkazi wa kijiji cha Makatapola Kata ya
Migoli Mzee asheri Mtwangula Masoya (60) akiuliza swali wakati wa
Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Makatapola jana.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Makatapola Meleji Sungula (kulia) akifuatilia mkutano.
0 maoni:
Chapisha Maoni