Jumapili, 24 Aprili 2016

JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA LATOA TAMKO KUHUSU BUNGE LA BAJETI


JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA LATOA TAMKO KUHUSU MWENENDO WA BUNGE LA BAJETI, LASIKITIKA WABUNGE WA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI KUTOKA UKUMBINI, LAPONGEZA VIKAO KUTOKUWA LIVE, LAIOMBA SERIKALI NAYO KUACHA KUONYESHA LIVE SHUGHULI ZAKE ZAIDI YA ZILE ZINAZOHUSIANA NA SIKU ZA MAPUMZIKO
Katibu wa Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania, Mtela Mwampamba akizungumza na waandishi wa habari leo, Ubungo mjini Dar es Salaam, kuhusu mwenendo wa Bunge la Bajeti na hatua ya Wabunge wa baadhi ya Vyama Vya upinzani kutoka nje ya ukumbi na kutotoa bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani. Kulia ni Mwanachama wa Jukwaa hilo, Simon Simalenga (Picha na Bashir Nkoromo).
 TAARIFA KAMILI NI IFUATAYO KAMA ILIVYOTOLEWA NA MWAMPAMBA
JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA (JUHWATA)
TAMKO JUU YA MWENENDO WA SHUGHULI ZA
BUNGE
Ndugu
wanahabari poleni na majukumu ya kulihabarisha Taifa, ndugu wanahabari tulio
mbele yenu ni wajumbe wa jukwaa huru la Wazalendo Tanzania ( JuhwaTa). Kama
mnavyojua jukwaa huru la WAzalendo ni taasisi huru inashughulikia mambo
mbalimbali ya kitaifa ikiwepo, Mijadala, Makongamano,Matamko na Elimu kwa umma
kuhusiana na mambo mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi kwa maslahi mapana
ya Taifa.
 
Leo
tumewaita, Jukwaa likiwa na masikitiko makubwa kuhusu mwenendo wa shughuli za
bunge, hususan bunge linaloendelea sasa pale Dodoma, bunge la bajeti, Kwa
mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
inalitaja bunge kuwa ndio chombo kikuu ambacho kitakuwa na madaraka , kwa niaba
ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika
utekelezaji wa majukumu yake
. Kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya wabunge
kususia mijadala,vikao na shughuli nyingine za bunge kwahiyo wamekuwa wakivunja
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 63 (2) na kutupelekea wananchi
kukosa fursa ya uwakilishi kutoka wa wale tuliwachagua huku wao wakiendela
kupata stahiki zao kwa maslahi yao.
Kwa mfano, Watanzania tunatambua
kwamba kuna baadhi ya wabunge walisusia bunge maalum la katiba matokeo yake
wananchi tukakosa mawazo mbadala kutoka kwao na walioumia ni wananchi wanyonge
na sio wao.


0 maoni:

Chapisha Maoni